Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Viongozi wa Wilaya ya Liwale alipowasili katika Viwanja vya Ujenzi Wilayani humo Mkoani Lindi kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa hadhara, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi katika Mikoa ya Kusini tarehe 17 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwa kuwahutubia wananchi wa Masasi Mkoani Mtwara tarehe 17 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mamwenye wa Masasi mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwa kuwahutubia wananchi wa Masasi Mkoani Mtwara tarehe 17 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Liwale katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Ujenzi Wilayani humo Mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi katika Mikoa ya Kusini tarehe 17 Septemba, 2023.
Viongozi na Wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Liwale wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya ujenzi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi katika Mikoa ya Kusini tarehe 17 Septemba, 2023.
Msanii Dula Makabila akitumbuiza kwenye Viwanja vya ujenzi Wilayani Liwale wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi katika Mkutano wa hadhara tarehe 17 Septemba, 2023.
Msanii Cholo Mwamba akitumbuiza kwenye Viwanja vya ujenzi Wilayani Liwale wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi katika Mkutano wa hadhara tarehe 17 Septemba, 2023.