Home BUSINESS PSSSF YAWAALIKA WANACHAMA, WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA 6 YA...

PSSSF YAWAALIKA WANACHAMA, WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA 6 YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

NA:K-VIS BLOG, GEITA.

WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wametakiwa kutumia fursa ya Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili vilivyopo eneo la Mamlaka ya Maeneo ya Usindikaji Nje (EPZA) mkoani humo Geita, kufika kwenye banda la Mfuko huo ili kuhudumiwa na kupata elimu inayohusiana na uanachama wao, Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Geofrey Kolongo, amesema.

Ameyasema hayo leo Septemba 22, 2023 kwenye banda la PSSSF, kwenye maonesho hayo ambayo PSSSF ni miongoni mwa taasisi za umma zinazoshiriki ili kuwahudumia wananchi na watumishi wanaoshiriki katika maonesho hayo.

“Tunatoa huduma zote ambazo zinapatikana kwenye ofisi zetu zilizoenea kote nchini, ambambo mwanachama ataweza kupata taarifa za Michango yake, taarifaz a Mafao yatolewayo na PSSSF, Wastaafu wataweza kujihakiki kwa njia ya biometric, lakini pia elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii, jinsi ya kutumia huudma za PSSSF kiganjani, na taarifa za uwekezaji.” Alisema Bw. Kolongo.

Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka, yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 23, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Biteko na yatafikia kilele Septemba 30, 2023.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu; Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 400

Previous articleWANANCHI KATA ZA LUHUNGA NA IHANU WILAYANI MUFINDI KUNUFAIKA NA UJENZI WA BARABARA YA IYEGEYA- LULANDA
Next articleTANZANIA KUBORESHA MFUMO WA USIMAMIZI NA UTOAJI WA TAARIFA ZA ANGA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here