Home BUSINESS ORYX GAS TANZANIA YAWA KAMPUNI BORA YA KIMATAIFA MWAKA 2023

ORYX GAS TANZANIA YAWA KAMPUNI BORA YA KIMATAIFA MWAKA 2023

Na: Mwandishi Wetu

ORYX Gas Tanzania imeshinda Tuzo ya Kampuni Bora ya Kimataifa ya Mwaka ambayo imetolewa na waandaaji wa Kongamano la Nishati Tanzania 2023.

Tuzo hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaaam wakati wa Kongamano hilo lililowakutanisha wadau wa sekta ya mafuta na gesi na Oryx imeshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza

Akitanza tuzo hiyo , Muandaaji wa Kongamano hilo la kimataifa, Abdulsamad Abdulrahim amesema kwa upande wa kampuni ya Oryx Energies ndio mara yake ya kwanza kupata tuzo hiyo kama kampuni ya kimataifa katika sekta ya nishati, ambayo imejitokeza katika kipindi cha miezi 12 iliyopita na kuchangia kibiashara na kiufundi katika kukuza sekta ya mafuta na gesi nchini Tanzania.

Abdulrahim ambaye pia ni Balozi wa heshima Brazil – Zanzibar na Mkurugenzi wa Ocean Business Patner ambao waandaaji wenza na DMG event kutoka London amefafanua tuzo hiyo pia inalenga kutambua uvumbuzi na Ubunifu kupitia biashara na ubunifu pamoja na kufanya mabadiliko mazuri katika sekta hiyo.

“Tuzo hii ni maalum kwa kampuni au Shirika ambalo lilitoa mchango bora kwa tasnia nchini Tanzania na kujidhihirisha kuwa kiongozi wa tasnia katika nyanja yoyote maalum ya sekta ya thamani ya mafuta na gesi.

” Kupitia maendeleo ya watu, kampuni ambalo lilipanua maarifa na kujifunza katika nyanja za kibiashara au kiufundi za sekta ya mafuta na gesi, “amesema Abdulrahim alipokuwa akielezea tuzo hiyo.

Akieleza zaidi amesem katika kutafuta mshindi, kura zilipigwa kupitia ukurasa wa Tanzania Energy Congress 2023 na Oryx Energies kuibuka kinara kwa mwaka huu 2023. “Hongera timu ya Oryx kwa mchango wa ajabu na mawazo ya ubunifu ili kuharakisha ukuaji wa sekta ya LPG nchini Tanzania.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Benoite Araman akizungumza kwa niaba ya timu nzima Oryx baada ya kupokea tuzo hiyo amesema Oryx Gas imefanya mengi sana kwa jamii kwa kipindi kifupi sana.

Ametoa mfano Oryx Gas imetoa mitungi na majiko zaidi ya 13,000 kwa wanawake toka makundi mbalimbali nchini Tanzania katika muendelezo ule ule wa Nishati safi ya kupikia kwa wote.

Ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kupitia REA kwa kutoa ruzuku kubwa kwa mitungi ya gesi kwa wananchi.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here