Home BUSINESS ORYX GAS, DORIS MOLLEL FOUNDATION WATOA ELIMU MATUMIZI YA GESI KWA JAMII...

ORYX GAS, DORIS MOLLEL FOUNDATION WATOA ELIMU MATUMIZI YA GESI KWA JAMII YA KIMASAI

KAMPUNI ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation imetoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya kupikia kwa baadhi ya koo za Kimasai wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Utolewaji wa elimu ya matumizi salama ya gesi katika Koo za Kimasai ni sehemu ya muendelezo ule ule wa kampuni ya Oryx kubadilisha maisha ya watanzania kuachana na nishati chafu na isiyo salama kwa matumizi ya kupikia na kuanza kutumia nishati safi hasa gesi.

Wafanyakazi wa Oryx Gas wakiongozwa na Meneja wa Masoko wa kampuni hiyo Peter Ndomba kwa kushirikiana na Doris Mollel foundation wamefika katika nyumba za koo za Kimasai na kuwafundisha matumizi salama ya nishati ya gesi.

“Tunafahamu jukumu ambalo tunalo kama kampuni ni kuendelea kutoa elimu ya matumizi salama ya majiko ya gesi, tumefanya hivyo katika makundi mbalimbali katika jamii ya Watanzania na leo hii kwa kipekee mafunzo haya tunayoa kwa koo hizi za Kimasai na tumetumia nafasi hii kuwapa elimu na kuwagawia bure mitungi ya gesi na majiko yake.”

Akieleza zaidi Ndomba amesema wanamshukuru Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel kwa jitihada zake za kuwafikisha Oryx katika boma za koo za Kimasai na kutoa elimu hiyo.

Amesisitiza Oryx itaendelea na mkakati huo kwa koo nyingine zaidi ili jamii yote ya Watanzania iweze kutumia nishati hiyo safi na bora kwa mapishi na kwamba utoa huo elimu pia umeenda sambamba na ugawaji mitungi ya gesi 300 kwa kada ya watumishi wa sekta ya afya wilayani Siha.

Previous articleRAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA ZIARA WILAYA YA RUANGWA
Next articleMABEHEWA YA SGR KUKAMILIKA KWA WAKATI KOREA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here