Home LOCAL NAIBU WAZIRI MWANAIDI AKABIDHI MIPIRA YA MAJI MPAPA ZANZIBAR NA. MWANDISHI WETU

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AKABIDHI MIPIRA YA MAJI MPAPA ZANZIBAR NA. MWANDISHI WETU

Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, akikabidhi mipira ya maji katika eneo la Mpapa Zanzibar, ambao walikuwa na changamoto ya maji, hii ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wakazi wa eneo hilo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na wakazi wa eneo la Mpapa Zanzibar wakati wa zoezi la kukabidhi mipira ya maji iliyotolewa na Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.

Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Kati Mhe. Khadija Kassim akitoa shukrani kwa Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis mara baada ya kukabidhiwa mipira ya maji katika eneo la Mpapa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wakazi hao, amekabidhi tarehe 26 Septemba, 2023.

Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis Pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga wakiwa katika picha ya Pamoja na wakazi wa eneo la Mpapa Zanzibar mara baada ya kukabidhi mipira ya maji kwa wananchi hao.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amekabidhi mipira ya maji kwa wakazi wa eneo la Mpapa lililopo Wilaya ya Kati ikiwa ni ahadi yake ya kutatua changamoto za upatikanaji wa maji katika eneo hilo.

Naibu Waziri Mwanaidi, amekabidhi mapema septemba 26, 2023 ambapo aliambatana na Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga huku akiwaeleza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati kuendelea kutatua changamoto mbalimbali katika jamii ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo ya maji.

“Niliahidi wakati wa ziara yangu, hii leo naitimiza kwa kukabidhi mipira hii, ili kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji, niwatakie kila lenye kheri katika kutunza mipira hii na endeleni kuiunga mkono Serikali yetu yenye nia dhabiti katika kuhakikisha uwepo wa huduma muhimu za kijamii,” alisema Mhe. Mwanaidi

Aliongezea kuwa, hii ni sehemu ya kuunga jitihada za Mhe. Rais ya kumtua mama ndoo kichwani na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi kwa kuondokana na changamoto zinazoweza kuwakwamisha katika utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga aliwakumbusha wakazi hao kuitunza mipira hiyo pamoja na kuwasihi kushirikiana kwa umoja katika masuala mbalimbali ya maendeleo nchini.

Naye Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Kati Mhe. Khadija Kassim akitoa shukrani kwa Naibu Waziri huyo alisema wamefarijika na kuendelea kuipongeza Serikali kwa kutatua changamoto zinazowakabili huku akitoa neno kwa wakazi hao kuunga mkono juhudi za Serikali yao.

“Binafsi naendelea kumpongeza sana Naibu Waziri Mwanaidi kuona umuhimu na kutuvusha katika hili, hii imekuwa historia kwetu, tunaona jitihada hizi kwa matendo siyo kwa huduma za maji tu, hata masuala ya afya, nishati na nyingine nyingi,”alisema Mhe. Khadija

Previous articleMSD: UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI UMEIMARIKA 
Next articleWANAFUNZI NYANKUMBU WANOLEWA NA GGML KUHUSU TAALUMA YA MADINI 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here