Home BUSINESS MRADI WA CLARITY WAWA LULU KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI NA AJIRA ZA...

MRADI WA CLARITY WAWA LULU KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI NA AJIRA ZA UTOTONI MIGODINI

.Na. Costantine James

Mradi wa CLARITY unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la VOS umekuwa na mafanikio makubwa Mkoani Geita kwa kusaidia kupunguza vitendo vya ukatili, ajira za utotoni kwenye migodi ya Uchimbaji madini ya dhahabu na kuwainua Wananchi kiuchumi.

Mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Geita na Mara ambapo kwa Geita unatekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Geita na Halmashauri ya Mji wa Geita sehemu ambazo zinashughuli nyingi za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini ya dhahabu Wanawake Mkoa Geita Bi Asia Hussein Masimba mmoja wa wanufaika wa mradi huo akiwa katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya teknolojia ya madini Geita amesema mradi huo umekuwa na manufaa makubwa katika eneo hilo.

Amesema kulikuwa na wimbi kubwa la ukatili kwa watoto wadogo kutumikishwa katika migodi baada ya familia zao kujengewa uwezo kiuchumi Hali hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa na sasa watoto hao wamerejea shuleni kupata haki yao ya msingi ya Elimu.

Mradi huo wa miaka mitatu kuanzia 2021/2023 unatekelezwa wa VSO kwa kushirikiana na wadau LEAT na TWCC nakwamba katika kipindi chote Cha mradi zaidi ya kesi Elfu Moja (1,000) za ukatili wa kijinsia ziliripotiwa na asilimia 75 ya kesi hizo walengwa wamepata haki zao.

Malengo makuu ya mradi huo ni kupambana na vitendo vya ukatili ikiwemo kutokomeza ajira za watoto migodini , kupambana na uharibufu wa mazingira katika maeneo ya Uchimbaji ikiwemo kurejesha Mazingira katika hali yake yaliyoharibiwa Kutoka na shughuli za utafutaji madini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here