Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Geita Gold Mining Limited (GGML) alipotembelea banda la kampuni hiyo leo Ijumaa.
Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania-GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akipata vipimo katika banda linalotoa huduma bure za uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume. Huduma hiyo imeratibiwa na Kampuni ya GGML kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.
Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania-GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) lililopo kwenye maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita..
NA: MWANDISHI WETU
MAKAMU Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti Tanzania-GGML anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo leo Ijumaa ametembelea maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kutoka kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo.
Mbali na kutembelea banda la Geita Gold Mining Limited (GGML) ambao ni wadhamini wakuu wa maonesho kwa mara nyingine mwaka huu, pia ametembelea banda la linalotoa huduma za elimu na uchunguzi wa saratani kwa wananchi wote mkoani Geita.
Banda hilo linalotoa huduma bure za uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume, limeratibiwa na Kampuni ya GGML kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.
Pia Shayo amepata maelezo kutoka kwa Mratibu wa huduma za Tiba Hospitali ya Rufaa ya mkoa Geita, Dk. Pasclates Ijumba ambaye amemueleza kuwa mbali na uchunguzi wa saratani hizo pia wananchi wataatiwa elimu ya kutosha namna ya kujikinga na maradhi hayo.
“Tunatoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hii hasa ikizingatiwa tatizo la saratani bado linakua kila mwaka hivyo ni vema kuwahi kufanya uchunguzi na kupata matibabu mapema na kuitibu kabisa lakini ukichelewa haitibiki na matibabu yake ni gharama kubwa kwa jamii yetu,” amesema.
Katika maonesho hayo ambayo mwaka huu yamejumuisha zaidi ya washiriki 400, yatafanyika kwa muda wa siku 10 kuanzia tarehe 20 hadi 30 Septemba mwaka huu.