Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AKIWASILI NCHINI HUNGARY

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI NCHINI HUNGARY

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Budapest nchini Hungary leo tarehe 13 Septemba 2023. Makamu wa Rais anatarajia kumwalikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Tano kuhusu Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) litakalofanyika tarehe 14-15 Septemba 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 13 Septemba 2023 amewasili Jijini Budapest nchini Hungary ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Tano wa Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) utakaofanyika tarehe 14-15 Septemba 2023.

Mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu ya “Dhima ya Familia: Msingi wa Usalama” utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watunga Sera, Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Dini na Wanataaluma.

Pia Mkutano huo unatarajia kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa, uhaulishaji wa teknolojia na uvumbuzi pamoja na ushirikiano katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo.     

                                            Franco Singaile

                           Msaidizi wa Makamu wa Rais – Habari

Previous articleRAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIHISTORIA MTWARA, LINDI
Next articleNDUMBARO ATOA MAAGIZO UKARABATI UWANJA WA MKAPA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here