Home LOCAL MAELFU YA WANANCHI MTWARA WAJITOKEZA KUMSIKILIZA RAIS SAMIA

MAELFU YA WANANCHI MTWARA WAJITOKEZA KUMSIKILIZA RAIS SAMIA

 
Na: Mwandishi Wetu, Nanyumbu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amepokelewa na maelfu ya wananchi wa Nanyumbu Mkoani Mtwara waliosimama barabarani kumsikiliza na kumsalimia.
 
Rais Samia ameendelea kupokelewa kwa kishindo na wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi katika ziara yake ya mikoa hii ya kusini.
 
Kila msafara wake unapopita, maelfu kwa maelfu ya wananchi wamejitokeza kumlaki, kumsikiliza na kumshangilia kutokana na maendeleo makubwa ambayo serikali yake imeleta kwenye mikoa ya kusini ndani ya miaka miwili tu.
 
Sekta za kilimo, miundombinu, umeme, maji, elimu na afya ni miongoni mwa maeneo ambayo yameshuhudia uwekezaji mkubwa wa serikali chini ya utawala wa Rais Samia kwenye Kanda ya Kusini na kwingine nchini.
 
Akizungumza na wananchi hao leo wilaya za Nanyumbu na Masasi, Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii.
 
Katika ziara hiyo Rais Dkt. Samia amepata wasaa wa kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi na kutoa nafasi kwa wawaziri wa sekta husika kutolea ufafanuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here