Home BUSINESS GST YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA MAONESHO YA MADINI JIJINI MWANZA

GST YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA MAONESHO YA MADINI JIJINI MWANZA

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imefanikiwa kuwa Mshindi wa Kwanza na kupata Tuzo katika kipengele cha Taasisi zinazohusiana na Madini.

Tuzo hiyo imetolewa na Chama cha Wafanyabiasha, Viwanda na Kilimo Tanzania (Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture) ambao ndiyo waandaaji wakuu wa Maonesho ya 18 ya Biashara Africa Mashariki yanayoendelea Jijini Mwanza katika Viwanja vya Furahisha.

GST imepata Tuzo hiyo katika maonesho hayo yaliyoanza Agosti 25, 2023 na yanatarajiwa kufikia kilele Septemba 04, 2023 ambayo yanabebwa na Kauli Mbiu isemayo “Mazingira Bora ya Biashara ni kitovu cha kukuza Uwekezaji wa Biashara, Viwanda na kilimo Afrika Mashariki,”.

Katika Maonesho hayo, GST imeshiriki kwa kuonesha huduma zitolewazo na taasisi hiyo ikiwemo aina ya miamba ya madini, huduma za maabara, Ramani za maeneo yapatikanayo madini na uchukuaji wa sampuli.

Previous articleRAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFURAHIA TAMASHA LA KIZIMKAZI ZANZIBAR
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 1,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here