Home LOCAL DKT. YONAZI WAKANDARASI KAMILISHENI MAJENGO YA MJI WA SERIKALI KWA WAKATI 

DKT. YONAZI WAKANDARASI KAMILISHENI MAJENGO YA MJI WA SERIKALI KWA WAKATI 

 NA: MWANDISHI WETU DODOMA

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewataka wakandarasi kuzingatia ubora katika ujenzi wa majengo ya Ofisi za Serikali katika eneo la Mtumba na kukamilisha kwa wakati.

Ametoa kauli hiyo alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali unaoendelea eneo la Mtumba Jijini Dodoma ambapo amekagua baadhi ya majengo ikiwemo la Ofisi yake, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Maji na Wizara ya Fedha.

Dkt. Yonazi amehizima kwa kila mkandarasi kuhakikisha anazingatia ubora na viwango vinavyotakiwa huku wakizingatia thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

“Dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona majengo haya yanakamilika kwa wakati na yawe na viwango vinavyotakiwa, bila kuwa na delays zozote ili kuhakikisha watumishi wote wanahamia haraka na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yao na kuliletea Taifa maendeleo yanayotakiwa,” alisema Dkt. Yonazi

Awali alipongeza kwa hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo na kueleza kuwa, Serikali imejipanga kuhakikisha hakuna mkandarasi atakayekwama kwa sababu zozote zile.

“Serikali imedhamiria kuona hakuna mikwamo katika ujenzi huu, hivyo msirudishe nyuma jitihada hizo, hakikisheni mnamaliza mradi huu kama ilivyoelekezwa,” Alisisitiza Dkt. Yonazi

Previous articleBASHE ATAKA WATANZANIA KUTUMIA AGRF KULETA TIJA KWENYE KILIMO
Next articleBENKI YA TCB YASHIRIKI KATIKA JUKWAA LA MIFUMO YA CHAKULA JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here