Home BUSINESS BENKI YA TCB YASHIRIKI KATIKA JUKWAA LA MIFUMO YA CHAKULA JIJINI...

BENKI YA TCB YASHIRIKI KATIKA JUKWAA LA MIFUMO YA CHAKULA JIJINI DAR

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kushoto), akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara (TCB), kwenye maonesho yanayoambatana na Jukwaa la Mifumo ya Chakula ((AGRF)), linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Septemba 5-8, 2023 Jijini Dar es Salaam.

TCB ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki Jukwaa hilo linalowaleta Wadau pamoja kujadilii hatua za kuboresha kilimo na mifumo ya chakula Barani Afrika.

Aidha Jukwaa hilo linalohudhuriwa na washiriki zaidi ya 4,000 kutoka katika Mataifa mbalimbali Duniani, ni la 13 kufanyika tangu kuanzishwa kwake, ambalo linatoa fursa kwa viongozi, wataalam, wabunifu na wadau mbalimbali kujadili masuala tofauti yanayohusu sera, changamoto, mafanikio na ubunifu utakaoboresha sekta ya kilimo na mifumo ya chakula.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa Mikopo Benki ya TCB Elisante Marir (wa pili kulia), alipokuwa kwenye Banda la Benki hiyo katika ziara yake ya kukagua Mabanda ya washiriki wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula linalofanyika Jijini Dar es Salaam.(wa kwanza kulia), ni Meneja Masoko wa Benki hiyo,Neema Rutatenekwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Benki ya TCB kwenye Banda lao. (kushoto), ni Meneja Mwandamizi wa Mikopo wa Benki hiyo, Elisante Marir, na (kulia) ni, Meneja Masoko wa Benki hiyo,Neema Rutatenekwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here