Home LOCAL ATUPWA JELA MIAKA 15 KWA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME ZANZIBAR

ATUPWA JELA MIAKA 15 KWA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME ZANZIBAR

Na: Halfan Abdulkadir, ZANZIBAR

Mahakama ya Mkoa Vuga Zanzibar imehukumu kwenda Jela Miaka 15 na kulipa Fidia ya Shil Milioni 1 mshtakiwa Haji Saleh Omar ( 20) Kwa kosa la Kumlawiti mtoto wa kiume Mwenye umri wa miaka 5.

Kosa Hilo ni kinyume na kifungu namba 115 (a) cha sheria ya adhabu namba 6/2018.

Akisoma hukumu hiyo Leo Sep 4, 2023, Hakimu wa mahakama hiyo Neyla Abdulbasit amesema Mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa Mahakamani Hapo kuwa hauna chembe ya shaka ndani yake.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani Hapo Desemba 22,2021 ambapo jumla ya Mashahidi 6 walitoa ushahidi wao katika mahakama hiyo na kusomwa hukumu dhidi ya Mtuhumiwa.

Vitendo vya ubakaji na Ulawiti Visiwani Zanzibar vimeendelea kuwa Kaa la moto Pamoja na kwamba Kesi hizi hazina dhamana, huku Miito ya Serikali, Wanaharakati na Viongozi wa kidini wakitaka adhabu zaidi itolewe kukomesha matendo hayo Visiwani humu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here