Home LOCAL RAIS Dkt. MWINYI ANA NIA YA DHATI YA KULETA MAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR...

RAIS Dkt. MWINYI ANA NIA YA DHATI YA KULETA MAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR – COMRED MBETTO

Na:Halfan Abdulkadir,Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema Rais wa Zanzibar  Dk Hussein Ali Mwinyi  ana nia ya dhati ya kufanya maendeleo ya kupigiwa mfano zanzibar na kuwatumikia  wananachi kwa usawa na haki.

Kimesisitiza ndiyo maana wananchi na CCM wana imani kubwa na aina ya uongozi  wake baada ya kubadilisha na kuipaisha Zanzibar Kimaendeleo, na kufanya Visiwa hivyo kuwa na haiba iliyobora.

Hayo yameelezwa na Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi na Uenezi Khamis Mbetto Khamis alipohojiwa na waandishi wa Habari Makao makuu ya CCM Zanzibar aliyopo Kisiwandui Mjini unguja. 

Mbetto alisema   kwa wiki kadhaa sasa Rais Dk Mwinyi alikuwa nje ya Nchi ambapo amesema si kwa ajili ya kutalii bali ni mawindo ya  kiuchumi ambayo yatailetea manufaa Zanzibar.

Mbeto Alisema ukiacha vikao vya ndani ya CCN kupima na kuridhika na uwezo wake wa kuwatumikia wazanzibari, rekodi ya utumishi wake wa umma wakati  aliposhika nyadhifa kadhaa ambazo ni nyeti kiongozi huyo amethibitika kuwa na utendaji unaozungatia sheria na utawala bora. 

“Chama chetu kina mikono na mizani ya kupima viongozi wake kama wanatosha au la. Vyombo vyetu vimelihalikishia taifa Rais Dk Mwinyi  ni mtu safi ,mzalendo na makini na hana makandokando katika nafasi zote alizowahi kuhudumu”Alisema  Mbetto. 

Aidha alisema chama na serikali  kinawahakikishia wananchi wote na kuwataka  waendelee kumuunga mikono kiongozi huyo Kwani ana nia thabit ya kuiletea zanzibar neema kama alivyoahidi katika uchaguzi mkuu 2020. 

“Wanaopiga kelele hivi  sasa majukwaani iko siku watayajujutia maneno yao . Watashindwa hata kumtazama usoni kwa aibu. SMZ ina mipango kabambe ya kuibadili na kuifikisha Zanzibar katika viwango vya kupigiwa mfano. “Alieleza Mbetto.

‘Tutaibadili Zanzibar kwa utelelezaji wa sera zetu na kuifanya zanzibar nchi ya mfano Afrika Mashariki. Wanaopiga kelele leo waweke na akiba ya maneno. Hakuna sababau itakayoifaya CCM isitimize ahadi zake mungu akipenda kwa wananchi “AliongezaMbetto

Itakumbukwa kuwa kauli ya CCM inakuja wakati ambapo ukishuhudiwa upotoshaji wa masuala ya Maendeleo unaofanywa na Wakosoaji wa kiongozi huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here