Home LOCAL Dkt. MWINYI: SERIKALI IMEFANYA JUHUDI KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI

Dkt. MWINYI: SERIKALI IMEFANYA JUHUDI KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI

Halfan Abdulkadir Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali imefanya juhudi za makusudi kudhibiti mfumko wa bei hasa kwa bidhaa za chakula nchini.

Aidha, imetoa agizo kwa wafanyabiashara wote wa vyakula kupunguza bei ya sukari ambayo ushuru wake kwa Zanzibar ni mdogo zaidi kuliko popote dunuani.

Dkt. Mwinyi amebainisha hayo Septemba 25,2023 Ikulu Zanzibar, alipokutana na wafanyabiashara mbalimbali nchini, wakiwemo wazalishaji, waagizaji bidhaa na mizigo, pamoja na wadau wote wa Biashara zikiwemo taasisi za Serikali na binafsi, ili kujadili mustakbali wa bei za bidhaa, hasa vyakula ziinazopanda bei kila uchao.

Aliwaeleza wanafanyabiashara hao kuwa karibu na kuzungumza na Serikali wakati wote kunapotokea matatizo badala ya kuwapandishia bei wananchi kwani wao ni waathirika wakubwa.

Akizungumzia suala la fedha sarafu ya dola Rais Dk. Mwinyi alizitaka mamlaka husika kutoa kipaumbele kwa wafanyabiashara wa chakula ili kuwaondoshea wananchi usumbufu wa uhaba wa chakula nchini.

Katika hatua nyengine Rais Dk. Mwinyi amewataka wafanyabiashara hao kuangalia uwezekano wa kuagiza bidhaa kwa pamoja na kuingiza nchini kwa wakati ili kuepuka gharama za usafirishaji na kuchelewa kuingiza vyakula nchini pamoja na kuwapa agizo la kushusha vyakula Pemba.

“Lazima kutafutwe njia ya kushushia vyakula moja kwa moja Pemba, mshirikiane kuchukua meli kutoka bandari ya Malindi hadi Pemba, kutafutwe ufumbuzi kwa njia yoyote ili kupunguza gharama za bidhaa madukani” Alisisitiza Rais Dk. Mwinyi.

Akizungumzia mabadiliko kwa Shirika la Bandari la Zanzibar Rais Dk. Mwinyi alieleza mabadiliko yoyote yanachangamoto zake, hivyo aliwataka wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano kwa uwekezaji mpya wa bandari hiyo na kuuagiza uongozi wa Shirika la Bandari kusimamia changamoto zinazojitokeza kwa kipindi hiki cha awali cha mkataba na wawekezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here