Home BUSINESS NAIBU WAZIRI KIGAHE AIPONGEZA BoT KUANZA KUNUNUA DHAHABU

NAIBU WAZIRI KIGAHE AIPONGEZA BoT KUANZA KUNUNUA DHAHABU

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe akipata maelezo kutoka kwa  Victoria Msina Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania BoT   kuhusu (BoT) kununua dhahabu wakati alipotembelea  banda la (BoT) katika  maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita,  Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho  Septemba 23, 2023 na Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la (BoT) katika maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita, kulia ni Victoria Msina Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho  Septemba 23, 2023 na Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe akioneshwa kitabu cha wageni ili kusaini kitabu hicho wakati alipotembelea  banda la (BoT) katika maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita, katikati ni Victoria Msina Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kulia ni Graciana Mahega Afisa Uhusiano Kwa Umma BoT,  Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho  Septemba 23, 2023 na Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe akitaka ufafanuzi kutoka kwa  Victoria Msina Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu BoT kununua dhahabu wakati alipotembelea  banda la BoT katika  maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita,  Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho  Septemba 23, 2023 na Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.

Baadhi ya wachumi na wataalamu wa fedha na mifumo ya fedha kutoka (BoT) wakiwa tayari kwa kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya Madini ya nayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe akipokea zawadi ya pochi ya kuhifadhia noti  kutoka kwa  Victoria Msina Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati alipotembelea banda la BoT katika  maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita,  Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho  Septemba 23, 2023 na Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe akitoa majumuisho ya ziara yake kwa waandishi wa habari mara baada ya kutembelea  banda la BoT katika maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita,  Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kesho  Septemba 23, 2023 na Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.

NA: JOHN BUKUKU, GEITA.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ipo katika mpango mahususi wa kuanza kununua dhahabu kwa ajili ya kuweka akiba ya kutosha ambayo itasaidia uchumi kuwa imara na kuleta tija kwa Taifa.

Akizungumza leo Septemba 22, 2023 katika Maonesho ya Madini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Bombambili Mkoani Geita, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, ameipongeza hatua hiyo na kusema kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wana programu mahususi ya kuanza kununua dhahabu ili kuwa na akiba ya kutosha katika kuhakikisha kunakuwa na uchumi imara.

Mhe. Kigahe amesema kuwa Serikali ipo tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kutokana ni wajibu wao kutoa msaada ili kuwainua kiuchumi.

Wazalishaji wa sekta ya madini wanapaswa kutumia fursa zilizopo kwa kutumia teknolojia sahihi, kufuata kanuni na taratibu za uchimbaji madini ili kuleta tija kwa Taifa”amesema Mhe. Kigahe.

Amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kunufaika na rasilimali ikiwemo madini na kujiletea maendeleo.

Hata hivyo amefurahishwa kuona madini ya dhahabu yanaongezewa thamani na kuwa katika viwango vya Kimataifa.

“Tunapaswa kuwa na dhahabu yenye viwango vyenye ubora asilimia 99.9, nawapongeza Wizara ya Madini kwa kufanikisha kazi hiyo” amesema

Amesema kuwa ili wachimbaji wadogo wa madini wapige hatua kiuchumi wanapaswa kuaminika kwa kujiunga na vikundi ili waweze kukopesheka na taasisi nyengine za fedha.

Ametoa wito wananchi kutoka Mikoa mbalimbali kushiriki katika ufunguzi wa maonesho ya madini ambayo yanatarajiwa kufunguliwa Septamba 23, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here