Home LOCAL RC CHALAMILA AWAPA NENO WAHARIRI WA HABARI AKIFUNGUA KIKAO KAZI CHA TMDA

RC CHALAMILA AWAPA NENO WAHARIRI WA HABARI AKIFUNGUA KIKAO KAZI CHA TMDA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila akizungumza alipokuwa akifungua kikao kazi cha Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na Wahariri wa Habari kilichofanyika leo Septemba 21,2023 katika Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo akizungumza alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi katika kikao kazi hicho kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kuwa vyombo vya habari vya mtandao vinapaswa kufanyakazi kwa kuzingatia taaluma ya habari ili kuongeza ufanisi kwenye kazi zao.

Chalamila ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi kilichoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na  Wahariri wa habari, kilichofanyika leo Septemba 21-2023 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa ni wazi kwamba Teknolojia imekua jambo linalopelekea wadau wa habari za mtandao kutumia fursa hiyo kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii, na kwamba kundi hilo linapaswa kusaidiwa kwa kuhakikisha wanatumia taaluma katika kazi zao ili waendelee kuaminika.

“Kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya waandishi wa mitandao, utakuta mwenye blog ndio muandishi na ndio mhariri, si dhani kama ni sawa na wao wanapaswa kufuata miongozo na taratitbu za utoaji habari kwa kuhakikisha wanatumia taaluma katika utoaji wa taarifa” amesema.

Ameeleza kuwa vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika jamii na Taifa kwa ujumla, na kwamba umakini zaidi unahitajika katika kuhabarisha umma ili kuepuka uvumi au uchochezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya  Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewezesha Mamlaka hiyo kuwa na vifaa vyenye ufanisi wa hali ya juu vinavyoweza kufanyakazi kwa haraka.

Ameeleza kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa mashine na mitambo katia maabara za TMDA, na kwamba, hiyo ni dhamira ya dhati ya Serikali katika kuhakikisha afya za watanzania zinalindwa wakati wote.

“Serikali imewezesha TMDA kuwa na vifaa ambavyo vinaweza kufanya kazi kwa haraka na kutoa majibu ya uhakika, hatua hii inasaidia kulinda afya za wananchi,” amesema Fimbo.

Baadhi ya Wahariri wa Habari na watendaji wa TMDA wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, albert Chalamila alipokuwa akizungumza katika kikao kazi hicho.

Meneja  Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Mamlaka ya Dawa na  Vifaa Tiba (TMDA) Gaudencia Simwanza akitoa neno la ukaribisho kwa Wahariri wa Habari waliohudhuria katika kikao kazi hicho.

Baadhi ya Wahariri wa Habari na Watendaji wa TMDA katika kikao kazi hicho.

Picha ya Pamoja. Kaimu Meneja Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Martha Malle, akitoa mada katika kikao kazi hicho kuhusu Sheria na Kanuni mbalimbali za udhibiti, za Mamlaka hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here