Mhe. Misengo Pinda ametembelea Banda la Chuo Kikuu hicho kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za kitaaluma na ubunifu.
Aidha amejulishwa kuhusu kampeni ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike Ndaki ya Mbeya na ameahidi kushiriki.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Rais Chakula na Kilimo Mh. Peter Mizengo Pinda akizungumza jambo na Dk. Nicholaus Tutuba Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ubunifu, Ujasiriamali na Ushirikiano wa Viwanda wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipotembelea Katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Jijini Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Rais Chakula na Kilimo Mh. Peter Mizengo Pinda akiangalia Bidhaa mbalimbali katika banda hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Rais Chakula na Kilimo Mh. Peter Mizengo Pinda akipata maelezo Kutoka kwa Bi. Gloria Mushi, Afisa Masoko Chuo Kikuu Mzumbe.