Home LOCAL KUNDI JIPYA LAIBUKA NGORONGORO, WATAKA WALIPWE FIDIA WAHAMIE WANAKOTAKA WAO

KUNDI JIPYA LAIBUKA NGORONGORO, WATAKA WALIPWE FIDIA WAHAMIE WANAKOTAKA WAO

Na. Mwandishi wetu

Zoezi la wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari hifadhini Ngorongoro limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa kundi jipya lenye mtazamo tofauti linalotaka kuruhusiwa kuhamia wanakotaka wenyewe kwa sharti tu la Serikali kuwalipa fidia zao na kuwahamisha

Baadhi ya wakazi wa vijiji kadhaa wenye mtazamo huo wanasema wao wapo kila sehemu Tanzania nakwamba ni vyema Serikali ikatoa uhuru huo wa wao kwenda wanakotaka

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Erkepusi Mbokieni Sapuo anasema yeye na familia yake wamechagua kwenda uelekeo wa Engaruka ambapo tayari kuna ndugu zao wengine wanaishi huko muda mrefu

“Tunaomba turuhusiwe kuhamia popote nje ya Ngorongoro bila ya kwenda Msomera.”

“Tunaiomba Serikali itupe fidia sisi tunataka kuhama lakini sio lazima twende kulikopangwa na Serikali.”

“Pawe na uhuru wa mtu kuchagua kama anataka kwenda Msomera sawa, kama anataka kwenda Kitwai sawa na kama hataki kwenda kokote kati ya huko sawa”.

“Mimi nataka niende maeneo ya Engaruka, Serikali inifidie niende na ndugu zangu.” Amesema Sepuo

Itakumbukwa kwamba tayari kaya zaidi ya 500 zimehama kwa hiyari kuelekea Msomera, Handeni mkoani Tanga na Serikali imetangaza kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa nyumba nyingine 5000 katika maeneo ya Msomera, kilindi na Kitwai Kwa ajili ya kuwahakikishia wakazi wa Ngorongoro wanaoendelea kujiandikisha Kwa hiyari.

Kuibuka kwa kundi hili linalotaka kuhamia mahala wanapotaka wenyewe ni mwendelezo wa kueleweka kwa zoezi hilo muhimu kwa UHIFADHI na Ustawi wa maisha yao.

Previous articleWATANZANIA WAPEWA WITO KUWAENZI WAASISI WA TAIFA
Next articleWAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA AAHIDI KUSHIRIKI UJENZI WA BWENI LA WANAFUNZI WA KIKE CHUO KIKUU MZUMBE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here