Home BUSINESS WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) MAONESHO YA NANENANE...

WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) MAONESHO YA NANENANE MBEYA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Nicodemus Mushi, (kushoto), wakati alipotembelea katika Banda la Mamlaka hiyo, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia), akizungumza jambo alipokuwa katika Banda la TPA, wakati wa ziara yake ya Kukagua Mabanda katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya. (kushoto), ni eneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Nicodemus Mushi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia), akipokea zawadi  kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa (TPA), Bw. Nicodemus Mushi alipotembelea katika Banda la mamlaka hiyo, kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Mwandishi wetu, MBEYA

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa wanatambua kazi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kutoa huduma za usafirishaji wa upokeaji wa mizigo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la TPA katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Amesema kuwa katika mipango ya Bandari ni pamoja na kushirikiana na  Sekta Binafsi katika kuongeza uwezo zaidi katika utoaji wa huduma.

Amesema kuwa katika kipindi hiki, Sekta Binafsi itasaidia kusukuma mbele sekta ya kilimo kwa kusafirisha mazao mbalimbali yanayozalishwa na wakulima wa ndani na wale wawekezaji katika sekta hiyo.

Aidha amesema kuwa serikali iko bega kwa bega katika kuhakikisha bandari inakwenda katika kuendelea kuongeza mapato na uchumi wa nchi.

Kwa Upande wake Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA Nicodemus Mushi, amesema kuwa TPA imeweza kuongeza miundombinu ya kisasa katika kuhudumia meli zinazoingia nchini.

Amesema katika hatua nyingine wanatarajia kujenga miundombinu kwa ajili ya mazao yatayokuwa yanasafirishwa nje ya nchi .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here