Home BUSINESS UTHUBUTU WA RAIS SAMIA UMENUSURU MFUKO WA PSSSF – KASHIMBA 

UTHUBUTU WA RAIS SAMIA UMENUSURU MFUKO WA PSSSF – KASHIMBA 

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba, katika mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania, ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, uliofanyika leo Agosti 31,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akizungumza kwa niaba ya Wahariri wa vyombo vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzani (TEF), akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba katika Mkutano huo.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo 

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba, amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika Mfuko huo, yanayokana na  uthubutu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kunusuru mfuko huo kwa kutoa zaidi ya shilingi Trilioni-4 kwaajili ya kulipia madeni ya mfuko huo.

Kashimba ameyasema hayo katika mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania, ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, uliofanyika leo Agosti 31,2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerer (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Katika kipindi cha miaka miwili, Rais Dkt. Samia, amelipa deni la michango la shilingi Trilioni-4.6 la wanachama uliyokuwa mfuko wa PSPF ya kabla ya mwaka 1999, ambapo uamuzi huo umewezesha mfuko kulipwa shilingi Trilioni-2.17 kupitia Hati Fungani.

“Serikali imelipa shilingi Bilioni-500 katika deni la shilingi Bilioni-731.4 la mikopo ya miradi ambayo mifuko minne iliyounganishwa ilikopeshwa ili kutekeleza miradi” ameeleza Kashimba.

Aidha ameeleza kuwa thamani ya uwekezaji ya mfuko huo wa PSSSF wenye zaidi ya wananchama 700,000, imeongezeka kwa Asilimia 23.5 kutoka shilingi Trilioni-6.40 hadi kufikia shilingi Trilioni-7.92.

Akizungumzia watumishi walioondolewa kazini kutokana na vyeti feki, Kashimba amesema kuwa, mfuko huompaka sasa mfuko huo umeshalipa jumla ya shilingi Bilioni-35 ikiwa ni michango kwa waliokuwa watumishi Elfu-13.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here