Home BUSINESS TMDA YASHAURI JAMII KUZINGATIA USHAURI WA WATALAAM WA AFYA  KABLA YA KUTUMIA...

TMDA YASHAURI JAMII KUZINGATIA USHAURI WA WATALAAM WA AFYA  KABLA YA KUTUMIA DAWA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi, Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. James Ndege (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kutembelea Mabanda ya Taasisi mbalimbali za Seriakli, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane, yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka (kushoto), akiagana na  Bw. James Ndege,  Afisa Mwandamizi, Elimu kwa Umma wa TMDA, Bw. James Ndege (kulia), mara baada ya kumaliza ziara yake katika Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeeya.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO) 

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeitaka jamii kutotumia dawa bila kufuata ushauri wa watalaam wa afya ili kulinda afya zao kwa kuwa matumizi holela ya dawa yanasababisha changamoto nyingi ikiwemo kusababisha usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa sanjari na ini na figo kushindwa kufanya kazi jambo linaloweza kusababisha vifo au afya kudhoofika.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Mwandamizi Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo, Bw. James Ndege wakati akielimisha makundi mbalimbali ya kijamii yaliyofika kupata elimu ya kazi za Taasisi hiyo kwenye banda la TMDA katika Maonesho ya Kimataifa ya  Nanenane yanayofanyika  kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Mamlaka hiyo inashiriki katika maonesho hayo ya kimataifa yanayofanyika jijini hapo kuanzia tarehe 1 – 8 Agosti, 2023 yakiwa na Kauli mbiu: “Vijana na Wanawake ni Msingi imara katika Upatikanaji Endelevu wa Chakula”.

“Bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyothibitishwa na TMDA ni muhimu katika kuokoa maisha ya watumiaji hata hivyo zikitumiwa bila kufuata ushauri wa wataalaam husika huweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya kama viungo vya mwili mfano figo na ini kushindwa kufanya kazi na wakati mwingine wagonjwa kupoteza maisha ama kuleta usugu wa vimelea kwa dawa zitakazotumiwa na jamii jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya wananchi na taifa. Hivyo ni muhimu wananchi wanapopata changamoto ya kuugua wafike katika vituo vya kutolea huduma ya afya kwa ushauri na uchunguzi na kutumia dawa kama watakavyoelekezwa”, alisisitiza Bw. Ndege.

Previous articleNAIBU WAZIRI KIGAHE AIPONGEZA OFISI YA MAKAMU WA KUANDAA KITABU CHA MUUNGANO
Next articleBENKI YA NMB YATENGA BILIONI 20 BBT, YAMWAGA MIKOPO KWA WAKULIMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here