Home LOCAL TMDA YACHAGULIWA KUWA KITIVO CHA KIKANDA UDHIBITI WA DAWA ZA CHANJO AFRIKA

TMDA YACHAGULIWA KUWA KITIVO CHA KIKANDA UDHIBITI WA DAWA ZA CHANJO AFRIKA

Na Mwandishi Wetu, Kiigali, Rwanda.

MAMLAKA ya Dawa na vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imechaguliwa kuwa Kitivo cha Kikanda katika udhibiti wa dawa za chanjo Barani Afrika katika mkutano wa taasisi za udhibiti wa dawa barani Africa (AMRC) mapema leo tarehe 24 Agosti, 2023.

Katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma kutoka TMDA, Chrispin Severe alipokea barua ya utambuzi wa TMDA kama Kitivo cha Kikanda (Regional Centre of Regulatory Excellence – RCORE) katika udhibiti wa dawa za chanjo kutoka kwa Mkurugenzi wa AUDA – NEPAD wa Utumishi na Maendeleo ya Taasisi za Udhibiti, Bw. Symerre Grey-Johnson.

Kwa TMDA kuchaguliwa kuwa RCORE imepewa nafasi baada ya kuhakikiwa na kuaminiwa kutoa msaada wa kiufundi, mafunzo na kujenga uwezo zaidi wa taasisi nyingine za udhibiti takriban 50 barani Afrika, ili ziweze kufikia viwango vya juu vya udhibiti ( kuanzia ML3) vinavyotambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Taasisi nyingine za udhibiti zilizothibitishwa na kupewa hadhi ya kuwa RCORE ni SAPHRA (Afrika Kusini), EDA (Misri) na FDA (Ghana).

TMDA ni taasisi ya kwanza Barani Afrika kufikia hatua ya ngazi ya tatu (ML3) toka mwaka 2018 kati ya ngazi 4 za WHO katika udhibiti wa dawa Dunuani.

Tanzania kupitia TMDA imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia kiwango hicho ambacho ni cha juu katika kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa dawa na vifaa tiba nchini katika kulinda afya ya jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here