Home BUSINESS SERIKALI YAWAALIKA WADAU WA SEKTA BINAFSI KUTOKA UINGEREZA

SERIKALI YAWAALIKA WADAU WA SEKTA BINAFSI KUTOKA UINGEREZA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, na ujumbe wake, wakifuatilia wasilisho wakati wa mkutano wake na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Worldline kutoka Ufaransa Bi. Caroline Jesequel, inayojihusisha na masuala ya utengenezaji wa mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao Ofisi Ndogo ya Hazina, jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bw. Japhet Justine, na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Huduma za Tehama, Dkt. John Sausi.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe.  Hamad Hassan Chande, akiteta jambo na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali Bw. Japhet Justine wakati wa kikao na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wordline kutoka Ufaransa Bi. Caroline Jesequel (hayupo pichani), Ofisi Ndogo ya Hazina, jijini Dar es Salaam.

Na. Josephine Majura, WF, Dar es Salaam

Serikali imewaalika wadau wa Sekta Binafsi kutoka Uingereza kuwekeza nchini ili kusaidia juhudi za Serikali kufikia malengo yake.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe.  Hamad Hassan Chande, alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey.

Mhe. Chande alisema Serikali imekamilisha utiaji saini na UK Export Finance kwenye  Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na kuendeleza barabara ya Tunguu – Makunduchi -kilomita 28, Fumba – Kisauni-Mazizini -kilomita 13.2, na mkoani – Chake Chake and Pemba Airport kwa ukubwa wa kilomita 43.5

Katika kikao hicho Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Chande aliwakaribisha Wawekezaji mbalimbali kutoka Uingereza kuja kuwekeza katika sekta za uzalishaji, uongezaji thamani na  utalii nchini Tanzania.

Nakukaribisha wewe na wafanyabiashara na wawekezaji wa kiingereza kuleta mitaji yenu Tanzania ” alisema Chande.

Kwa upande wake Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey Humphrey, alisema watashirikiana na Serikali kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika na kuendekeza kuwekeza katika vipaumbele vya kibiashara vilivyopo nchini Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here