Naibu Waziri, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kighahe akizungumzia alipokuwa akisoma hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apomuwakilisha katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara la Watendaji Wakuu wa Makampuni na Taasisi mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Makampuni na Taasisi mbalimbali wakifualia hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyosomwa na Naibu Waziri, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Biashara la Watendaji Wakuu wa Makampuni na Taasisi mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kighahe ( wa pili kulia) akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya watendaji wa Taasisi mbalimbali (hawamo pichani), wakati wa Mkutano huo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kighahe (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Jukwaa la Biashara la Watendaji Wakuu wa Makampuni na Taasisi mbalimbali wakati wa Mkutano wa Jukwaa hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM
Serikali imesisitiza kuendelea kuboresha mioundombinu, mazingira ya kushirikiana na taasisi za sekta binafsi katika Biashara na uwekezaji.
Hayo yamebainishwa kwenye hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, iliyosomwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kighahe (Mb), katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara la Watendaji Wakuu wa Makampuni na Taasisi mbalimbali (2000 CEO’s Business Forum) uliofanyika mwishoni mwa wiki hii Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kigahe amesema kuwa Ushirikiano imara uliopo baina ya Sekta Binafsi na Umma umeongeza chachu katika maendeleo ya nchi na kwamba kumewezesha kuimarika kwa Mifumo itakayoleta matokeo chanya kwa Taifa.
“Ni ukweli usiopingika kuwa ushirikiano imara wa sekta ya umma na sekta binafsi umekuwa chachu ya maendeleo hapa nchini, hivyo basi inapaswa kuwekwa mifumo imara ya ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi Ili kufikia kilele cha mafanikio ya Taifa letu kwa kuweka mazingira bora ya ukuaji wa uchumi jumuishi kwa mafanikio ya kila mmoja wetu.
“Ni muhimu sana kuweka mkazo wa ushirikiano wenye tija baina ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.” amesema na kuongeza kuwa.
Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya kufanya Biashara nchini kwa lengo la kufanikisha dhamira ya Serikali ya kufanya kazi na Sekta Binafsi nchini.
“Tunatambua matarajio ya wafanyabiashara wakuu na viongozi wa Taasisi wa sekta waliopo hapa leo. Napenda mfahamu kuwa tutashirikiana na wadau mbalimbali katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza pamoja na kutumia fursa zilizopo katika kutatua changamoto hizo.” amesema Mhe. Kighahe.
Hata hivyo ameongeza kuwa Serikali inahitaji ushirikiano na Sekta Binafsi binafsi ili kutekeleza miradi ya kitaifa na ya kimkakati kama ujenzi wa mioundombinu mbalimbali kama barabara, madaraja na reli ya kisasa SGR.