Home LOCAL SERIKALI IMEDHAMIRIA KUONDOA CHANGAMOTO YA UMEME URAMBO – CHATANDA

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUONDOA CHANGAMOTO YA UMEME URAMBO – CHATANDA

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu Hassan imeweza kutatua changamoto ya umeme katika Wilaya ya Urambo na Mkoa wa Kigoma ambapo zaidi ya Bilion 30 zimeletwa katika kuhakikisha zinajenga Kituo Cha Kupoza Umeme katika Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Akizungumza leo katika Ziara ya Wilaya hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amewapongeza Kampuni ya TBEA_ CHINA na uwongozi wa Tanesco na Serikali kwa ujumla kwa kusimamia kikamilifu mradi huu ambao utakuwa chachu ya kuondoa Changamoto za umeme katika baadhi ya Vitongoji.

Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali ya awamu ya sita inalengo la kuondoa hadha ya umeme kwa wananchi wake katika kuhakikisha wanapata umeme kila sehemu na kwasasa niwaombe wananchi kuhakikisha mnalinda Miundombinu ya umeme katika maeneo yenu.

“Nimeona maeneo mengi uwa wanachoma moto nguzo hivyo niwaombe wananchi wangu kuwa makini na kulinda Miundombinu ya Tanesco katika maeneo yenu ili Serikali hizidi kuleta fedha nyingi na kuepusha umeme kuzimika zimika.”

Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda amefurahishwa na ajira ya vijana ambao wanafanya katika Ujenzi huo wanatoka katika Wilaya ya Urambo na Wilaya jirani za Mkoa wa Tabora kwa kuwa sisi kama Viongozi tunahimiza kuwajali na kuthamini wazawa ambao wapo katika eneo la mradi ili wawe chachu ya kuwa walezi wa Mradi huo.

“Mwenyekiti Chatanda amewasii vijana ambao wamepewa ajira hapo kuwa waaminifu na waadilifu katika kulinda vifaa na Miundombinu iliyopo katika mradi huo ili mradi umalize kwa wakati na uwe bora zaidi .”

UWT IMARA JESHI MAMA KAZI IENDELEE

Previous articleTANZANIA, INDIA ZAIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI
Next articleTWIGA MINERALS CORPORATION KINARA TUZO YA UTOAJI BORA WA GAWIO KWA SERIKALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here