Home LOCAL MTENDAJI MKUU BRELA AKIPONGEZA CHUO KIKUU MZUMBE UJENZI WA BWENI LA WANAFUNZI...

MTENDAJI MKUU BRELA AKIPONGEZA CHUO KIKUU MZUMBE UJENZI WA BWENI LA WANAFUNZI WA KIKE MBEYA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, (wa pili kushoto), akitia saini katika Kitabu cha wageni alipofika kwenye Banda la Chuo Kikikuu Mzumbe, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane katika Viwanja vya John Mwakangale Agosti 7,2023Jijini Mbeya. (wa kwanza kushoto), ni Bw. Aloyce Gervas Mwakilishi wa Kurugenzi ya Ukimataifaji na Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe Gervas, na (wa kwanza kulia), ni Afisa Masoko Chuo Kikuu Mzumbe, Gloria Mushi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa (kulia), akipokea zawadi ya Kikombe kutoka  Mwakilishi wa Kurugenzi ya Ukimataifaji na Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas, huku akipata maelezo juu ya Mradi wa ujenzi wa Bweli la Wanafunzi wa Kike linalojengwa katika Ndaki ya Mbeya.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, (katikati aliyekaa) akiwa na jopo la baadhi ya watumishi, na wanataaluma wa Chuo Kikuu Mzumbe mara baada ya kumaliza ziara yake fupi katika Banda la Chuo hicho, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane Agosti 7,2023 Jijini Mbeya

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here