Home BUSINESS MHE.MARY MASANJA ATEMBELEA PORI LA AKIBA MPANGA KIPENGERE MKOANI NJOMBE

MHE.MARY MASANJA ATEMBELEA PORI LA AKIBA MPANGA KIPENGERE MKOANI NJOMBE

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ametembelea Pori la Akiba Mpanga Kipengere Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutangaza utalii na kukagua utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Amefanya ziara hiyo tarehe 9 Agosti, 2023.

Mhe. Masanja amehamasisha watanzania kutembelea pori hilo lenye vivutio mbalimbali vya kihistoria, utamaduni, maporomoko ya maji na mandhari nzuri.

Aidha, amemuelekeza Mkuu wa Hifadhi hiyo Donasian Makoi kuendelea kutangaza vivutio vya pori hilo pamoja kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha kwa watalii wanaofika katika eneo hilo kufika bila bughudha.

Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Mpanga Kipengere Donasian Makoi amesema hifadhi hiyo ilianzishwa kutokana na umuhimu wake kiikolojia kwa kuwa chanzo cha maji cha mabonde ya Rufiji na Nyasa.A

meongeza kuwa jumla ya miradi 10 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.7 imetekelezwa ambapo nyumba za wageni 12 ya watalii, njia ya miguu kwa watalii, daraja moja, barabara yenye urefu wa kilomita 13, kambi ya watalii, lango la utalii, jengo la ofisi na nyumba ya askari vimejengwa.

Hifadhi ya Mpanga Kipengere ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 1,574.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here