Home LOCAL MDAHALO WA WANAJAMII KUHUSU MWITIKIO WA VVU NA UKIMWI KUFIKIA MALENGO YA...

MDAHALO WA WANAJAMII KUHUSU MWITIKIO WA VVU NA UKIMWI KUFIKIA MALENGO YA KIMATAIFA YA MWAKA 2023

NA: MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) kanda ya Dar es Salaam limevitaka vituo vya kutolea huduma za VVU na UKIMWI (CTC) kufanya kazi kwa muda wa saa 24 ili kuongeza upatikanaji wa huduma.

Maagizo haya yalitolewa jijini Dar es Salaam Jana wakati wa mdahalo wa wadau na kundi la wanaume kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam uliolenga la kujadili na kubainisha mitazamo mbalimbali ya jamii juu ya changamoto ya VVU na UKIMWI.

Mdahalo huo pia ulilenga kubainisha makundi yaliyosahaulika au yasiyofikiwa katika jitihada za kupambana na UKIMWI, pamoja na mchango wa jamii katika kuongeza kasi ya kupambana na UKIMWI ili kufikia malengo endelevu ya mwaka 2030.

Katika mdahalo huo, makundi kadhaa yaliyobainika kusahaulika na kukosa huduma na elimu kuhusu VVU na UKIMWI, makundi hayo ni pamoja na Wafugaji ambao huishi kwa kuhama-hama, wafanyakazi wa saluni za kiume, watumiaji dawa za kulevya wanaoshirikiana mabomba ya sindano, Wasichana wa kazi za majumbani, Wanawake wanaojihusisha na biashara za ngono katika maeneo ya vijijini, Viongozi wa dini pamoja na Watu wenye ulemavu wa kusikia na kunena ambao wanakabiliwa na changamoto za kimawasiliano.

Kutokana na kuwepo kwa makundi ya watu wengi ambao hawafikiwi na elimu ya UKIMWI, washiriki wa mdahalo huu waliazimia kuongeza uwezo wa kongamano ili kuweza kufikia watu wengi zaidi, Kuendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, pamoja na Kuzingatia umuhimu wa usiri wa taarifa za wapokea huduma ili kupunguza utoro wa dawa.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here