Home LOCAL MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Rehema Sombi, amesema wapo baadhi ya watu wamekuwa chanzo cha migogoro katika jamii na kuwavunjia heshima viongozi wa kitaifa jambo ambalo halikubaliki na linapaswa kukemewa.

Amesema kukabiliana na tatizo hilo ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwalea na kuwakuza watoto katika maadili mema yenye kuheshimu mila, utamaduni na viongozi wa nchi.

Rehema ameeleza hayo leo Agost 26, 2023 Dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha ‘Rais wa Kwanza Mwnamke’ (The First Female President) kilichoandikwa na mtoto Arafat Simba.

“Watu hao wamekuwa wakiwachochea wengine kuvunja uaminifu kwa taifa lao sambamba na kuvunja heshima za viongozi wa kitaifa, wanaotumia matamshi ambayo yanatweza utu wa viongozi wetu.

“Kinachoshangaza hao viongozi wa jamii wanashindwa kutumia nafasi zao kukanya matendo yanayokwenda kinyume na maadili na uzalendo wa taifa, badala yake wanatumia nafasi zao kukwamisha juhudi za maendeleo zinazowekwa na serikali,” amema.

Previous articleSUA YAFANYA MAZUNGUMZO NA WAJUMBE WA TUME YA HAKI JINAI.
Next articleHAWA HAPA WATAKAONUFAIKA NA UFADHILI WA MABILIONI YA RAIS SAMIA SEKTA YA AFYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here