MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Rehema Sombi, amesema wapo baadhi ya watu wamekuwa chanzo cha migogoro katika jamii na kuwavunjia heshima viongozi wa kitaifa jambo ambalo halikubaliki na linapaswa kukemewa.
Amesema kukabiliana na tatizo hilo ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwalea na kuwakuza watoto katika maadili mema yenye kuheshimu mila, utamaduni na viongozi wa nchi.
Rehema ameeleza hayo leo Agost 26, 2023 Dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha ‘Rais wa Kwanza Mwnamke’ (The First Female President) kilichoandikwa na mtoto Arafat Simba.
“Watu hao wamekuwa wakiwachochea wengine kuvunja uaminifu kwa taifa lao sambamba na kuvunja heshima za viongozi wa kitaifa, wanaotumia matamshi ambayo yanatweza utu wa viongozi wetu.
“Kinachoshangaza hao viongozi wa jamii wanashindwa kutumia nafasi zao kukanya matendo yanayokwenda kinyume na maadili na uzalendo wa taifa, badala yake wanatumia nafasi zao kukwamisha juhudi za maendeleo zinazowekwa na serikali,” amema.