Home BUSINESS MABALOZI WA TANZANIA NJE YA NCHI KUIBEBA SEKTA YA MADINI

MABALOZI WA TANZANIA NJE YA NCHI KUIBEBA SEKTA YA MADINI

Leo Agosti 30, 2023.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewapokea Waheshimiwa Mabalozi Wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania nchini Canada, Namibia, Austria, Oman na Ufaransa jijini Dodoma.

Ziara hiyo ya Mabalozi imelenga kufahamishwa kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini nchini.

Katika kikao hicho Mabalozi watapata taarifa kutoka katika taasisi za Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Taasisi za Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), STAMICO, TEITI na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Mabalozi hao waliotembelea Wizara ya Madini ni Balozi Joseph Sokoine anayekwenda Canada, Balozi Fatma Rajab- anayekwenda Oman, Balozi Naimi Azizi- anayekwenda Austria, Balozi Ali Jabir Mwadini – anayekwenda Ufaransa na Balozi Ceaser Waitara -anayekwenda Namibia.

Previous articleMAADILI YA VIONGOZI NI MSINGI WA UONGIZI BORA – MHANDISI MAHUNDI
Next articleMBIBO AWAOMBA MABALOZI KUISAIDIA WIZARA KUTIMIZA NDOTO ZA WAASISI SEKTA YA MADINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here