Home LOCAL KINONDONI MFANO BORA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA MAJI

KINONDONI MFANO BORA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA MAJI

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea na kukagua mradi wa usambazaji maji kutoka Makongo hadi Bagamoyo uliotekelezea na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA ) katika kata ya Mivumoni na kuridhishwa na kazi iliyofanyika kuwafikishia wananchi huduma ya maji.

“Nipende kumshukuru Mh.Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya katika sekta ya maji, mradi huu ni mfano wa mapinduzi makubwa katika sekta ya maji nchini. Nikiri kuwa Wilaya ya Kinondoni hapo awali ilikua na changamoto kubwa ya maji hasa eneo hili la Mivumoni lakini kwa sasa maeneo mengi wanapata huduma ya maji kwa saa 24.”ameeleza Mheshimiwa Maryprisca.

Ameongeza kuwa huduma bora ya maji kama ilivyoboreshwa katika Wilaya ya Kinondoni ndio dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwa vitendo na ndio dhamira ya Wizara ya Maji kuona kila eneo huduma ya maji inafika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na DAWASA katika utekelezaji wa mradi huo na kumhakikishia Mhe Naibu Waziri kuwa malalamiko ya Maji yanakwisha Wilaya ya Kinondoni yamekwisha.

“Maeneo machache ambapo makazi Mapya yanaendelea kujengwa tunaamini kuwa huduma itafika kwa wakati, kwa sasa kazi ya maunganisho ya maji inaendelea na kila kaya itapata huduma ya maji” ameeleza Mh.Mtambule

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji maji DAWASA, ambaye pia ni kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Shaban Mkwanywe amemshukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kwa kuidhinisha fedha za utekelezaji wa mradi huo zaidi ya Tsh Bilion 65 zilizoenda kumaliza kilio cha upatikanaji wa huduma kwa wilaya tatu ambazo zimenufaika na mradi huu ambazo ni Wilaya ya Kinondoni, Ubungo na Bagamoyo.

Nae Mkazi wa Mivumoni ndugu Shani Ally ameishukuru Serikali kwa mradi huu wa maji ambao umewapunguzia gharama za maisha kwa kiasi kikubwa.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia maji ya chumvi na kununua maji kwa gharama kubwa, lakini sasa maji haya ambayo tunayapata katika makazi yetu ni nafuu sana kwetu,” ameeleza ndugu Shani.

Previous articleMAMA MARIAM MWINYI: WANAWAKE WAJAWAZITO TUMIENI MWANI KUIMARISHA AFYA ZENU
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 20-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here