Home LOCAL KINANA:TAMASHA LA KIZIMKAZI CHACHU KUIMARISHA MUUNGANO

KINANA:TAMASHA LA KIZIMKAZI CHACHU KUIMARISHA MUUNGANO

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Ndugu Abdulrahman Kinana, amesema Tamasha la Kizimkazi limefanikiwa kuwa chachu ya kuimarisha Muungano.

Kinana amesema hayo Agosti 31, 2023, alipozungumza kwenye Tamasha la Nane la Kizimkazi, Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti amesema, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wa nchi, amedhirisha uongozi ni kuonyesha njia katika nyanja zote.

“Nchi yetu imepata maendeleo makubwa katika nyanja zote,” alisema Ndugu Kinana katika tamasha hilo lililopambwa na kazi za utamaduni, sanaa na kuhudhuriwa na halaiki ya watu.

Ndugu Kinana alisema, kwa ukubwa na umaarufu wa tamasha hilo, siyo shughuli ya Zanzibar tu, bali ni tukio ambalo limeweka misingi mizuri ya kuimarisha Muungano.

Amefafanua kwamba, tamasha hilo kwa mwaka huu limewavuta Watanzania wengi kutoka nje ya Zanzibar kushiriki, na siku zijazo wengi zaidi watamiminika Kizimkazi siyo tu kujionea bali kushiriki.

Ameongeza kusema kuwa, kuna matamasha mengi, katika nchi mbalimbali na kutoa mfano wa Brazil, Italia,  India,  Uhispania na Ireland; na kwa namna Tamasha la Kizimkazi lilivyofana, linaelekea kuwa la viwango vya kimataifa .

 “Shughuli hii nadhani imeanza kama miaka mitatu hivi, lakini kwa namna tunavyoiona, itakuja kuwa ya kimataifa, itaingia kwenye kalenda ya dunia na watu wote duniani watapanga tarehe za kuja Kizimkazi,” alisema Ndugu Kinana.

     

Previous articleBENKI YA CRDB YAPONGEZWA KWA HATIFUNGANI YA KIJANI YENYE RIBA YA ASILIMIA 10.25 INAYOTOA FURSA YA UWEKEZAJI KWA WOTE
Next articleEWURA YATEKELEZA AZMA YA UTAWALA BORA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here