Home LOCAL KATIBU MKUU DKT. YONAZI AMEONGOZA KIKAO CHA JIMBO LA SERIKALI

KATIBU MKUU DKT. YONAZI AMEONGOZA KIKAO CHA JIMBO LA SERIKALI

NA: MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha Jimbo la Serikali kilichofanyika tarehe 24 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Serengeti uliopo Jengo la Ushindani Dar es Salaam.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD),

Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu, na Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia (Global Fund).

Aidha, kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) ambacho wajumbe wake ni Jimbo la Serikali, Asasi za Kiraia (NSA), na Wadau wa Maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here