Home LOCAL DP WORLD : KKKT YAUNGA MKONO UWEKEZAJI, YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HEKIMA

DP WORLD : KKKT YAUNGA MKONO UWEKEZAJI, YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HEKIMA

Arusha, Agosti 21, 2023

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo, amesema kuwa kanisa lake lina imani na namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan analisimamia suala la uwekezaji kwenye bandari na kumpongeza Rais kwa uongozi wake wenye hekima.

Kanisa la KKKT limesema kuwa linamuunga mkono Rais Samia na linaunga mkono uwekezaji nchini.

KKKT pia imekemea watu wanaotaka kuligawa taifa kupitia kwa mjadala unaoendelea wa bandari kwa maslahi yao binafsi ya kidini, kisiasa na kiuchumi.

Zifuatazo ni kauli 10 nzito zilizotolewa na KKKT kupitia kwa Askofu Mkuu Dk Shoo:

1. “Lipo hili la DP World Mheshimiwa (Rais). Kwanza naomba lieleweke wazi kwamba kanisa linaunga mkono uwekezaji. Hatupingi uwekezaji Mheshimiwa Rais”

2. “Tunajua wewe (Rais) kwenye nia yako unataka wawekezaji”

3. “Sisi viongozi wa dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni kabisa mwa jambo hili (mjadala wa DP World) na kwa uungwana wako na kwa unyenyekevu ulionao na utayari wa kusikiliza, ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama taasisi na viongozi wakuu wa dini katika nchi yetu ya Tanzania. Madhehebu yote ya Kikristo, tukiwa CCT, tukiwa TEC na tukiwa BAKWATA. Mimi nakumbuka jinsi ulivyotupokea, ukatusikiliza. Ukapokea maoni yetu na ushauri wetu viongozi wa dini na ukaahidi kuwa maoni na ushauri hayo utayapeleka kwa wataalamu na kufanyiwa kazi kwa uzito kwa maslahi mapana ya taifa”

4. “Tuna imani na wewe Mheshimiwa Rais

Previous articleDKT. KIRUSWA: STAMICO HAKIKISHENI MNAIMARISHA SEKTA YA CHUMVI NCHINI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 22-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here