Home INTERNATIONAL DKT. TAX AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA COMORO

DKT. TAX AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA COMORO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta za kipaumbele hususan bishara na uwekezaji, afya, uchukuzi, elimu, utamaduni, uchumi wa buluu na maeneo mengine.

“Tanzania itaendelea kushirikiana Comoro ili kuendeleza ushirikiano uliodumu kwa kipindi kirefu kwa maslahi ya pande zote mbili hususan katika sekta za biashara na uwekezaji,” amesema Dkt. Tax

Kwa upande wake Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed amesema kwamba Comoro inajivunia kuwa na uhusiano imara na Tanzania ambapo uhusiano huo umekuwa imara na umedumu kwa muda mrefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here