Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Dkt.. Eliza Mwakasangula, akizungumza na waandishi wa habari katikaMaonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale JIjini Mbeya.
Maofisa wa Chuo Kikuu Mzumbe wakizungumza na vijana waliotembelea katika Banda lao kufahamu Programu mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo MBEYA.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Dkt. Eliza Mwakasangula amesema kuwa Chuo hicho kimeendelea kutoa elimu Bora na inayowasaidia wanafunzi kumudu soko la ajira, na kuweza kujiajiri wenyewe mara wanapohitimu masomo yao.
Ameyasema hayo Agosti 1, 2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale JIjini Mbeya,
Amesema kuwa ushiriki wao katika Maonesho hayo ni kuhabarisha Umma juu ya huduma wanazozitoa na hasa upande wa mafunzo na kutzitangaza Programu zao mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho.
“Tupo kwenye Maonesho ya Nanenane kuzungumza na wananchi kuwaeleza Programu zetu ambazo zimekuwa zikiwasaidia sana wahitimu wetu kuweza kujitegemea na kujiajiri wenyewe, pia kukidhi ushindani uliopo kwenye soko la Ajira” amesema Bi. Mwakasangula.
Kwa upande wao Baadhi ya Vijana waliotembelea katika Banda la Chuo hicho, wameonesha kufurahishwa na Programu zinazotolewa na Chuo hicho na kusifu mpangilio mzimo wa namna Ada za masomo zinavyopangiliwa na kugawanywa kwa muhula na nakufanya ulipaji wake kuwa rahisi.