Baadhi ya wanavikundi vinavyoshiriki NaneNane kwa udhamini wa Barrick Bulyanhulu wakionesha bidhaa wanazozalisha katika banda la Maonesho la Barrick lililopo katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Afisa Mahusiano ya umma wa Barrick Bulyanhulu,Mary Lupamba, akielezea programu za mgodi za kuwezesha wajasiriamali wadogo kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi huo.
Bidhaa za asali zinazozalishwa na wanavikundi wanaowezeshwa na Barrick Bulyanhulu.
Baadhi ya wanavikundi vinavyoshiriki NaneNane kwa udhamini wa Barrick Bulyanhulu wakionesha bidhaa wanazozalisha katika banda la Maonesho la Barrick lililopo katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanavikundi vinavyoshiriki NaneNane kwa udhamini wa Barrick Bulyanhulu wakionesha bidhaa wanazozalisha katika banda la Maonesho la Barrick lililopo katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanavikundi vinavyoshiriki NaneNane kwa udhamini wa Barrick Bulyanhulu wakionesha bidhaa wanazozalisha katika banda la Maonesho la Barrick lililopo katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu
-Yashirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Msalala kuwezesha vikundi vya wajasiriamali kushiriki maonesho ya Nane Nane Simiyu
Simiyu : Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya kilimo nchini, na kupanua masoko kwa ajili ya wakulima na wafugaji, kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, imewawezesha wawakilishi kutoka vikundi 11 vya wajasiriamali wanaofanya shughuli zao za kilimo na ufugaji katika maeneo ya jirani na mgodi huo kushiriki katika maonesho ya nane nane kanda ya ziwa mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Akizungumza katika maonesho hayo afisa mahusiano ya jamii wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba, amesema kuwa mara nyingi wakulima na wafugaji huzalisha bidhaa mbalimbali lakini hukabiliwa na changamoto ya soko la bidhaa zao.
“Sisi kama mgodi kwa kushirikiana na halmashauri ya Msalala tumeonelea kwamba maonesho haya ya nane nane ni fursa na ni eneo ambalo lina wananchi wengi na wadau wengi wa kilimo na ufugaji tukaona ni vizuri tuweze kuja nao kwa ajili ya wao wenyewe pia kujifunza masuala mengine ya kilimo na mifugo na kutengeneza mitandao ya masoko ya bidhaa zao”, amesema Lupamba.
Aidha ameeleza kuwa wawakilishi hao waliofika katika viwanja hivyo wamenufaika na fursa mbalimbali zilizopo viwanjani hapo.”Wametembelea mashamba mbalimbali ya mifano yaliyopo katika viunga hivi vya Simiyu, wameweza kujifunza jinsi ya kuzalisha kwa tija bidhaa mbalimbali pamoja na ufugaji”,amesema Lupamba.
Lupamba amesema mbali na kuwezesha wajasiriamali kushiriki maonesho mbalimbali kwa ajili ya kupanua wigo wa masoko yao pia mgodi wa Barrick Bulyanhulu umesajili zaidi ya wajasiriamali 40 kutoka vijijini jirani na mgodi kwenye mfumo wa zabuni wa mgodi kwa ajili ya kuuza bidhaa zao mgodini pia umekuwa ukiwawezesha kwakuwapatia mafunzo ya ujasiriamali ambapo mpaka sasa yameishawafikia wajasiriamali zaidi ya 500.
Akiongea kwa niaba ya wajasiriamali wenzake waliowezeshwa kushiriki maonesho ya Nane Nane, Hussein Malimi,amesema maonesho haya ni moja ya fursa kwao katika kuongeza mtandao wa masoko na kujifunza mambo mapya. “Ujio wangu hapa katika maonesho haya umeniwezesha kukutana na watumiaji wapya wa bidhaa zangu za asali na wenzagu wameweza kuuza bidhaa zao na kupata oda mpya”,alisema Hussein.
Kwa upande wake, Samuel Igoko, ambaye pia anajishughulisha na ufugaji wa nyuki amesema fursa ya kushiriki maonesho hayo imempa nafasi ya kujitangaza na kupanua zaidi soko la bidhaa zake.
“Tunashukuru kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa kutuwezesha kufika hapa na kushiriki maonesho haya, yametuwezesha kukutana na watu wengi na kujitangaza na hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wa Barrick katika eneo letu unazidi kutunufaisha wananchi”, amesema Igoko.
Maonesho ya nane nane kanda ya ziwa mashariki yanafanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu tangu Agosti Mosi hadi Agosti nane mwaka huu.