Home BUSINESS WATANZANIA TUCHANGAMKIE FURSA KUTOKA IRAN

WATANZANIA TUCHANGAMKIE FURSA KUTOKA IRAN

Na:Neema Adriano

Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE  Bi. Latifa Mohamed Khamis amewaasa Watanzania kuchangamkia fursa za biashara katika nchi ya Iran

Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Taifa la Iran katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Sabasaba yanayofanyika Katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

“Huu ni wakati Watanzania kubadili uwelekeo kwa kuchangamkia fursa zilizopo Irani hususani katika sekta ya kilimo, afya, teknolojia na elimua Ambapo katika sekta ya kilimo Tanzania tuna fursa za kupeleka Ufuta, ngano na mafuta, ni fursa nzuri ambayo wakulima wetu wanapaswa kuichangamkia ili waweze kunufaika nayo.

“Kwa upande wa Afya pia wenzetu wametuzidi vitu vingi, tumeshafanya maongezi na ubalozi wa Iran hapa nchini na wamekubali kuleta madaktari wao ambao kutakuwa na kambi maalum kubadilishana utaalamu wao na madaktari wetu, teknolojia wanazotumia na sisi basi hatimae tuweze kupiga hatua zaidi katika matibabu.” Amesema.

Hivyo amewataka Watanzania wafikirie Iran kwa ajili ya kufanya nao kazi, vizuri katika suala la huduma kwa wateja, gharama kufanya biashara Irani sio ghali, ni Dola 100 ukibadilisha unapata zaidi ya elfu Hamsini hivyo watanzania wanaweza kwenda kubadili upepo wa kibiashara ili waweze kupata mabadiliko ya kibiashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here