Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka akipokea zawadi ya kibebeo cha maua kilichotengenezwa kwa shanga kutoka kwa Bw. Kadaso Kipingili wa UDOM
Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka akipata maelezo kutoka kwa Bi. Betlanda Msola kutoka UDOM kuhusu programu za Shahada za Juu.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka (aliyeketi katikati) katika picha ya pamoja na wafanyakazi alipotembelea banda ya UDOM.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof Lughano Kusiluka, amewahimiza wananchi kutembelea maonesho ya 47 ya Kimataifa SABASABA, na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa UDOM ambao pia wanashiriki maonesho hayo.
Prof Kusiluka ameyasema hayo leo tar 2 Julai 2023, alipotembelea maonyesho hayo jijini Dar es salaam, ambapo miongoni mwa mabanda aliyotembelea ni Banda la watu wa China, UDSM, Mzumbe na TTCL.
Mara baada ya kuwasili, Prof. Kusiluka alipata fursa ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Maonesho na ukuzaji wa biashara wa TANTRADE, Bw. Fortunatus Mhande, ambapo alipendekeza mbinu bora za kuendelea kutumia viwanja hivyo nje ya maonesho ya Sabasaba, pamoja na kupata maoni ya wadau kuhusu namna nzuri ya kuendelea kuboresha maonesho hayo ili yaendelee kuwa na ubora wa Kimataifa.
Prof Kusiluka alihitimisha ziara yake kwa kutembelea banda la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), na kuona mambo mengi yaliyopo kwenye banda hilo ikiwemo bunifu mbali mbali zinazoweza tatua changamoto mbalimbali kwenye sekta ya Afya, Kilimo na Ardhi. Amewapongeza Wafanyakazi wote walioshiriki maonesho hayo na kuwataka kuendelea kutoa Huduma Bora na yenye weledi kwa Wananchi wanaotembelea UDOM, pamoja na kukusanya maoni ya namna ya kuendelea kuboresha maonesho yajayo.