Home Uncategorized WANANCHI WAFURIKA MKUTANO WA CCM SINGIDA

WANANCHI WAFURIKA MKUTANO WA CCM SINGIDA

Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi  katika mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo katika  Uwanja wa Bobandia Mjini Singida Julai 23,2023.

Katika mkutano huo wa leo wa Kanda ya Kati inayojimuisha mikoa ya  Tabora, DODOMA na Singida, pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu Chongolo ataelezea hatua kwa hatua  usahihi wa makubaliano ya uwekezaji kwa ajili ya kuboresha uendeshaji na ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa viwango vya hali ya juu tofauti, ili kuongeza, tofauti na ilivyo sasa.

Ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Stephen Wassira na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Ndugu Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Ujenzi na  Uchukuzi, Atupele Mwakibete na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Jerry Silaa.

(Picha na Richard Mwaikenda) 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here