Home BUSINESS WANAFUNZI VETA PWANI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KUTENGENEZA NEMBO KWA KOMPUTA

WANAFUNZI VETA PWANI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KUTENGENEZA NEMBO KWA KOMPUTA

Veta Pwani waja na mradi mpya ya kutengenezea Mashine ya kudalizi na kutengeneza nembo au maumbo mbalimbali kwa kutumia komputa ambayo yatawekwa kwenye mashine yoyote

Akizungumzia kuhusu mradi huo, mwalimu kutoka katika Chuo hicho Necsory Kayombo amesema wao hufundisha mwanafunzi kutengeneza nembo au maua mbalimbali ya pembeni na kuweka kwenye mashine ambayo inafanya kulingana na ulivyoielekeza.

“Kwa mfano inavyoonekana hapa hii nembo ambayo tayari imeshatengenezwa unaweza ukaweka kebo au flashi na kuiamishia kwenye mashine ambayo huku unapanga kabisa Uzi na upande huu mwingine zinapangwa kwa namba, inafanya kazi mpaka ikimaliza Uzi au ikikata Uzi au ikimaliza kazi.

“Machine hizi zinapatika Nchi tofauti tofauti lakini sisi hii tumechukua Korea hivyo tunaandaa nguvu kazi ambayo itasaidia Kijana kwenda kuajiriwa au kujiajiri,” amesema Kayombo

Kozi nyingine zitolewazo katika Chuo hicho Cha veta Pwani ni pamoja na ushonaji kuanzia levo 1 mpaka 3,Umeme wa magari na WA majumbani,maabara pamoja na sekretari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here