Home LOCAL WAMI /RUVU KUKABILINA NA UKAME.

WAMI /RUVU KUKABILINA NA UKAME.

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.

Bodi ya Maji Bonde la Wami /Ruvu imeiomba kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Morogoro kusaidia kutokomeza shughuri za kibinadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji hasa kuelekea kipindi cha ukame kiangazi ili kunusuru vyanzo hivyo ambavyo hutililisha Maji yake katika Mto Ruvu ambao utegemewa kutoa huduma ya Maji Dar es salaam, Pwani na Morogoro.

Ombi hilo limetolewa kwenye kikao maalumu kati ya Bodi ya Maji Bonde la Wami /Ruvu na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Morogoro ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Rebeca Nsemwa kwa ajili ya kujadili kwa pamoja jinsi ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Akizungumza nje ya kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Elibarik Mhandisi Mmassy amesema vyanzo vya Maji vilivyo kwenye Safu ya Milima ya Uluguru inatakiwa kulindwa kwani ndio inategemewa kujaza maji kwenye mito zaidi ya mitano ambayo inajaza Maji Mto Ruvu.
“Kipindi cha ukame kinachangamoto nyingi ikiwemo shughuli za kilimo, ufugaji pamoja na uchechuaji wa Madini kwenye mito, sasa hivi vitu vikichanganyika kwa pamoja vinaleta changamoto kubwa sana kwenye vyanzo vyetu vya Maji, hivyo tumeshirikisha kamati ya Ulinzi na Usalama ili kuona jinsi gani hizi shughuli haziharibu vyanzo vya Maji”. Alisema Mkurugenzi Mtendaji.

“Tumepitia katika vipindi vigumu mfurulizo katika miaka miwili, hivyo tumeamua tujipange mapema, ili jambo lililo tokea Mwaka Jana na Mwaka Juzi lizitokee au litokee kwa athari dogo sana “. Aliongeza.

Akitoa taarifa ya hali ya Maji Meneja Rasilimali za Maji Bodi ya Maji Bonde la Wami – Ruvu Martine Kasambala amesema kuna ongezeko la mahitaji ya Maji kwenye Shughuli za Kilimo, Mifugo, Madini na Viwanda ukilinganisha na uwezo wa vyanzo kwa sasa.

Amesema kwa matumizi ya Mamlaka, Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam ( DAWASA) inatumia mita za ujazo 500.000 kwa siku, Wakala wa maji Vijijni ( RUWASA) 61.500 pamoja na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Morogoro ( MORUWASA) 34.000.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Rebeca Nsemwa Afisa Tawara Wilaya ya Morogoro Hilary Sagara amesema kamati hiyo itashirikiana na Wami – Ruvu kutatua changamoto ya uharibifu wa vyuanzo vya maji unatokana na shughuli za Kibinadamu kwenye safu ya milima ya uluguru.

Previous articleWANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABASABA)
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 4,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here