Na: Neema Adriano, Dar-es-Salaam
Waandishi wa Habari kutoka chama Cha waandishi wa habari Dar-es-Salaam (DCPC) wamejengewa uelewa kuhusu maswala ya kidigitali na usalama wa kidigitali.
Akizungumza Julai 19, 2023 wakati wa mafunzo hayo ya siku Moja mkufunzi wa mafunzo hayo Francis Nyonzo amesema wanafanya uchachamuzi katika haki za kidigitali kwa hiyo mara kwa mara wamekuwa wanatoa mafunzo ya usalama wa kidigitali na kuhusu haki za kidigitali.
“Leo tumefenya hayo maswala ya usalama kidigitali na tumegusia kidogo kuhusu haki za kidigitali hii ni kama sehemu ya vitu ambavyo vimekuwa tukisimamia miaka yote tumekuwa na makundi mbalimbali tukiyapatia uelewa wa maswala ya kidigitali hii kwa sababu digitali haiepukiki.
“Sasa hivi watu wengi wanaingia katika mwaswala ya kidigitali kama tunavyoona Sasa hivi Kuna data za mwezi wa sita,zinaonyesha kwamba vifaa milioni 34 vimeungamishwa kwa hiyo ni zaidi ya nusu ya Watanzania wameunganishwa na mtandao hivyo Kuna haja ya Watanzania kufahamu namna ya kuwa salama mtandaoni.
“Kwa hiyo katika makundi ambayo tunawapa ufahamu ni waandishi wa habari tunafahamu kuwa waandishi wanawasiliana na watu wengi kwa hiyo tunatamani kuona kunawa na habari nyingi zinazohusu maswala ya kidigitali na usalama wa kidigitali kwa sababu muda mrefu watu wamekuwa wakipata matatizo kwa sababu ya kutokufahamu haki za kidigitali, kutokufahamu namna ya Kujiweka salama mtandaoni.
“Maswala ya utapeli yamekuwa yakiendelea kwa sababu Watu hawajui namna ya kujilinda mtandaoni na tumeona madhara ya watu kununua simu zilizotumika na mtu mwingine zilizotumika au kuokota laini ya mtu mwingine na kuitumia bila kujua alikuwa akiitumia kwa matumizi yapi,hupelekea watu kupata madhila ya kukamatwa,” amesema Nyonzo.
Pia amewataka waandishi wa habari kujikita zaidi katika kuandika habari za kijamii na za kiuchunguzi kuliko kukimbilia habari za matukio.
Nae Katibu kutoka chama Cha waandishi wa habari Dar-es-Salaam,Fatma Jalala ameishukuru Jamii forums kwa kutoa mafunzo hayo na ameuomba uongozi uendelee kutoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari.
“Nashukuru Sana Jamii forums kwa mafunzo ambayo imetupatia hivyo basi tunaomba waendelee kutupatia mafunzo haya na tunaahidi kuyatekeleza,”amesema.