Bw Baraka Munisi
Taratibu za kuunganisha taasisi mbili za kifedha za Letshego Tanzania, (Letshego Tanzania Limited t/a “Faidika” na benki ya Letshego Tanzania) umekamilika na kuzaliwa taasisi mpya ya kifedha ya Benki ya Letshego Faidika “Letshego Faidika Bank”.
Bodi ya Wakurugenzi ya Letshego Group imemteua Bw Baraka Munisi kushika wadhifa wa Afisa Mtendaji Mkuu Benki mpya ya Letshego Faidika.
Bw. Baraka Munisi alijiunga na ‘Faidika’ ambayo ilikuwa chini ya kampuni ya Letshego mwaka 2018, na Mei, 2019, aliteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa ‘Faidika’ mwaka mmoja baadaye.
Ndani ya miaka mine chini ya uongozi wa Bw Baraka, taasisi ya Faidika iliweza kuongeza maradufu shughuli za mikopo midogo midogo, kuongeza ufanisi wa uendeshaji na kuwa taasisi ya kwanza ya Microfinance Tanzania kupata leseni ya daraja la pili (II) ya kuchukua amana.
Bw Simon Jengo ambaye ni mwenyekiti mpya wa bodi ya Benki mpya ya Letshego Faidika, amethibitisha uteuzi wa Bw Munisi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu. Jengo alisema “Utendaji wa Letshego nchini Tanzania utafungua fursa nyingi za wadau na sasa tunaweza kuongeza ufanisi wa biashara, huku tukiwapa wateja wetu machaguo mbalimbali ya bidhaa zetu ambazo ni matokeo ya kuunganisha taasisi hizi mbili.
Kupitia uongozi wa Bw. Baraka katika taasisi ya Faidika na hasa kwa kuzingatia taaluma na uzoefu wake wa kitaifa na kimataifa, tunatarajia malengo yetu yanatafanikiwa na kufanya mageuzi makubwa na maendeleo ya biashara nchini Tanzania.”
Kupitia mazingira mazuri ya uwekezaji nchini na utendaji kazi wa taasisi hii mpya, tunarajia kudumisha na kuendeleza kauli mbiu ya Benki ya Letshego Faidika ya #ImaraPamoja au #StrongerTogether.
“Ni heshima kubwa kupata fursa ya kuendelea kuongoza taasisi ya Letshego Tanzania kupitia awamu nyingine yenye lengo la kukuza na utoaji huduma bora kwa wateja wetu nchi nzima.
Tutaendelea kutumia rasilimali za biashara zote mbili ili kufikia malengo yetu ya kuboresha maisha ya Watanzania.
Hakika sisi tupo #ImaraPamoja, imara kama timu iliyoungana na shukrani kubwa zaidi kwa ushirikiano wa kimkakati tulioanzisha na mashirika mbalimbali ya Tanzania.
Mkakati wa Benki ya Letshego Faidika unabaki kuwa ule ule wa kuleta ukuaji endelevu wenye ufanisi mkubwa wa kijamii kwa vizazi vijavyo,” alisema Bw Munisi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu mteule wa Tanzania wa Benki ya Letshego Faidika.
Uwepo wa benki ya Letshego Faidika utaendeleza shughuli zao mbalimbali za Letshego ambazo ni ukopeshaji, akiba, bima, malipo na mtindo wa maisha ambapo ambapo wateja watakuwa na fursa ya kupata huduma mbalimbali kwa njia za kisasa zaidi kupitia tovuti, USSD, huduma za simu za mkononi na WhatsApp).
“Taasisi yetu ya Afrika Mashariki itafaidika kutokana na kuunganishwa kwa taasisi hizi mbili na kuwa taasisi moja yenye dira na madhumuni ya kuleta ufanisi wa kifedha na fursa kwa Watanzania popote.
Kama shirika la Afrika nzima, uboreshaji wa duduma mbalimbali endelevu unabakia kuwa muhimu katika kuimarisha biashara na kuendelea kutoa thamani kwa wateja wetu katika nchi 11 barani Afrika,” alisema Fergus Ferguson, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Masoko ya Mashariki na Magharibi wa Letshego Group.
Ujumuishaji wa mashirika mawili ya Letshego katika Benki ya Letshego Faidika unaanza kutoka 04 Julai 2023, huku timu za eneo na nchi za chapa hiyo zikiwa zimeunganisha mifumo, mitandao, utawala na bidhaa zote kwa muda wa miezi 18 iliyopita. Wateja sasa wanaweza kufikia chaguo pana zaidi katika bidhaa, na wanaweza kutazamia matoleo ya kusisimua zaidi katika siku zijazo.
Kwa sasa Watanzania watashuhudia ubadilishaji wenye maboresho makubwa ya matawi na maduka ya Letshego na kuwa na muonekano mpya wa rangi ya njano na nyeusi ambayo ni rangi halisi ya benki ya Letshego Faidika ikiwa na kauli mbiu ya #ImaraPamoja ikiwa na nembo ya yenye rangi ya njano na pembetatu a ‘tripod’ inayoashiria uaminifu, usaidizi na ukuaji.
Matawi na sehemu za kutolea huduma pia yataunganishwa au kuhamishwa ili kuongeza urahisi kwa wateja upata huduma bora mbalimbali za mfumo wa kidigitali.
WASIFU WA BW BARAKA MUNISI.
Bw. Baraka Munisi alijiunga na Letshego kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018 akiwa kama Mshauri kiongozi, na mwaka 2019, aliteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya kifedha ya Faidika chini ya kampuni ya Letshego. Chini ya uongozi wa Bw Munisi, Taasisi ya Faidika iliongeza faidi maradufu huku ikipnguza gharama mbalimbali kwa njia ya utendaji kazi ulioimarishwa na kuwa taasisi ya kwanza ya Taasisi ndogo ya Fedha Tanzania kupata leseni ya kuweka amana ya daraja la II.
Bw Munisi pia alifanikiwa kuleta uzoefu wa kimataifa wa masuala ya fedha na kibenki kwa zaidi ya miaka 18 katika jukumu lake jipya ambapo aliupata akiwa mfanyakazi katika mashirika kadhaa ya umma na kimataifa.
Kabla ya kujiunga na Letshego, Bw Munisi aliwahi kufanya kazi katika kampuni mbalimbali ambazo ni Freddie Mac USA ambayo ni moja ya ya mashirika mawili ya Serikali ya Marekani, JP Morgan Chase USA, Wells Fargo USA, Benki ya Dunia; na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Katika kipindi chake katika Benki ya Dunia Bw. Munisi alichukua jukumu muhimu katika kuanzisha kituo cha kwanza cha ukwasi wa mikopo ya nyumba katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kiitwacho Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC). Akiwa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Munisi alihusika na utekelezaji wa Mradi wa Kitaifa wa Fedha kwa ajili ya makazi.
Pia alikuwa muhimu katika kuanzisha mpango wa kitaifa wa makazi ya watumishi wa umma, chini ya agizo la Rais wa Tanzania wakati huo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Baada ya hapo alisaidia uanzishwaji wa ‘Watumishi Housing’, taasisi inayomilikiwa na Serikali inayomilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa Tanzania ili kutoa nyumba za gharama nafuu kwa watumishi wa umma.
SIFA: (ELIMU)
Bw Munisi kwa sasa ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Biashara, fedha na Makazi aliyohitimu katika Chuo cha Biashara cha Kogod Schools of Business and International Management in Washington DC); Pamoja na shahada zingine toka Chuo cha Wharton Business School of Real Estate Pennsylvania Philadelphia; Boulder institute of Microfinance Turin, Italia; Chuo Kikuu cha Frankfurt, Ujerumani.