Home BUSINESS UJUZI NA UMAHILI UNAOTOLEWA NA CHUO CHA BAHARI, KUWAKWAMUA VIJANA NA UKOSEFU...

UJUZI NA UMAHILI UNAOTOLEWA NA CHUO CHA BAHARI, KUWAKWAMUA VIJANA NA UKOSEFU WA AJIRA

    

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam, (DMI), Dkt.Tumaini Gurumo, amesema kuwa Chuo hicho kimejikita katika kutoa elimu bora inayowawezesha vijana kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira.

Dkt.Gurumo ameyasema hayo katika maohojiano maalumu kwenye Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Amesema vijana wengi wamekuwa wakivutiwa kujiunga na Chuo hicho kutokana na umahilri wake katika fani mbalimabali wanazotoa za Bahari, ikiwemo kozi ya Ubaharia.

Aidha pamoja na mambo mengine, pia Chuo hicho kimejikita kutoa mafunzo kama mafuta na gesi, pamoja na ufundi wa mitambo mbalimbali mikubwa. ikiwemo mitambo ya melini.

“Tuna huduma zote hapa katika Banda letu, wale ambao hawajatambua nini wanataka hasa fani ya kusoma, basi wakifika hapa tutaweza kuwashauri vizuri kutambua ni eneo gani linaweza kuwafaa, hasa kwa mtazamo mzima wa maendeleo ya nchi yetu katika uchumi wa bluu.

“Hivyo basi, nawakaribisha, usajiri unaendelea na masomo yanakwenda kuanza mwezi Octoba mwishoni au Novemba mwanzoni” amesema Dkt Gurumo.

Ameongeza kuwa Chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Cheti hadi Shahada ya Uzamivu, na kwamba, mafunzo wanayotoa yanawapa vijana ujuzi utakaowawezesha kufanyakazi katika sekta ya Bahari ambayo imeendelea kukua na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

“Tanzania meli zinaendelea kujengwa hivyo zinahitaji waendeshaji, na heti tunachotoa katika Chuo chetu kinampa nafasi ya kuweza kupata kazi Duniani”

“Kwa upande wa Baharia, Cheti anachopata mhitimu wetu kinamsaidia kupata kazi moja kwa moja Baharini” ameongeza Dkt.Gurumo na kusema, pia Chuo hicho kinatoa kozi kuanzia wiki tano, na baada ya hapo anakwenda moja kwa moja baharini kufanya mazoezi.

Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo, “Kukuza ujuzi nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa uchumi imara na shindani” yameshirikisha Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu zaidi ya 80 ambapo, yanatarajiwa kuhitimishwa rasmi Julai 22, Mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here