Home BUSINESS TTCL YAZINDUA AKAUNTI PEPE KURAHISISHA HUDUMA ZA FEDHA

TTCL YAZINDUA AKAUNTI PEPE KURAHISISHA HUDUMA ZA FEDHA

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetekeleza dhana ya ukuaji wa uchumi kidigitali Kwa kuzindua akaunti ya kidigitali ya kuweka na kutoa fedha ijulikanayo kama akaunti pepe Kwa kutumia simu janja ya mkononi.

Kwa kutumia akaunti hiyo haimlazimishi mteja kuwa na Kadi ya benki badala yake atatumia simu ya mkononi.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade) Latifa Khamis amezindua akaunti hiyo july 9 iliyobuniwa na TTCL katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam amesema Kwa kutumia akaunti hiyo mteja alazimiki kuwa na akaunti ya benki badala yake anapaswa kuwa na simu janja pekee.

Amesema ubunifu uliofanywa na TTCL ni wa kipekee kwa kufungua akaunti inayotumika na simu janja ya mkononi ,huduma ambayo imekuja kwa wakati muafaka wa matumizi ya kidigitali.

“Ni huduma iliyokuja wakati muafaka,ikirahisisha upokeaji wa fedha,ikichochea biashara mdogondogo na kubwa,” amesema Latifa na kuongeza kuwa ni mfumo unaosaidi kutotmbea na fedha (cashless) na kuongeza usalama wa fedha pia.

Amesema akaunti hiyo inatumiwa na wateja wote wa mitandao ya simu za mkononi ambapo inafungua fursa zaidi Kwa wananchi.

Amesema TTCL imeleta mapinduzi makubwa kwa sekta hiyo ikirahisisha wasiokuwa na akaunti katika benki kuweza kutumia mfumo huo na kunufaika na usalama wa fedha.

” Ni mfumo wenye kuchochea uchumi na kukuza sekta ya fedha lakini pia inachochea uwekezaji,” amesema Latifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa T-Pesa,Lulu Mkude amesema uzinduzi wa akaunti hiyo ni wa kipekee wenye na kuleta maendeleo makubwa ya teknolojia ambapo inatoa fursa kushiriki uchumi wa kidigitali.

Amesema itachochea maendeleo ya uchumi ambapo inatumika kupokea,kutumia fedha, kulipa bima mbalimbali na manunuzi ya kidigitali ambapo pia ni ya Kila mmoja.

Amesema mteja anaweza kujiunga na kufurahia huduma za kifedha za kidigitali na kinachotakuwa mteja kuwa na simu janja ya mkononi na kupakua mfumo huo kupitia simu yake kupitia T-Pesa App na kufuata mtiririko kisha akaunti hiyo kufunguliwa.

Amesema ni akaunti ya kurahisisha huduma za kifedha ambayo ni hatua muhimu katika kukuza huduma za fedha.
Mwishoo

Previous articleSHAWEJI AWATAKA UWT KINONDONI KUANZA MAPEA MAANDALIZI YA UCHAGUZI
Next articleRAIS SAMIA:TUTAIWEZESHA JKT KUWA YA KISASA NA KUENDANA NA MAHITAJI YA SASA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here