Na: Neema Adrian, Dar-es-Salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu kuhusu ulipaji Kodi na kupata huduma mbalimbali zitolewazo na mamlaka hiyo
Akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya 47 ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ya Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya ndani TRA Ndositwe Haonga amesema kuwa amefika hapo ili kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi na wadau wao wanaofika kwa ajili ya kupata huduma.
Amesema wanazo huduma mbalimbali ikiwemo misamaha ya Kodi kwa mtu yoyote au Taasisi ambayo inaweza ikawa na shida au mahitaji hayo kutaka kujua ni namna gani zinapatikana na ni jinsi afanye au afate hatua Gani basi wanaweza kufanya hivyo.
“Lakini pia tumekuja kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutoa Kodi na kuhimiza kwa mfano Kodi yetu hii tunayoitoa ndio hiyo hiyo inatumika kwenye huduma za jamii mfano,Afya,Elimu,maji na miundo mbinu mbalimbali.
” Sasa hivi Serikali yetu hii inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan ni Serikali ambayo umejikita kuboresha huduma mbalimbali na wengi ni mashahidi Huduma za miundo mbinu imeboreshwa ikiwemo maji, barabara, mashule, Afya vyote vimeboreshwa kwa hiyo nitoe wito kwa wadau wetu tunayo Ile kauli mbiu yetu ya kwamba ukitoa Hela dai risiti hivyo basi wafanya hivyo kwa kuwa hiyo Kodi ndio inatoyotumia kurudisha huduma kwa jamii,” amesema Haonga.
Kwa upande wa Maadili amesema kuna dawati linalosimamia maswala ya Maadili kwamba kwa Sasa TRA Haina mchezo kwenye swala Zima la Maadili mtu yoyote asisite Wala asiache kulipoti kwenye dawati na kupata maelekezo Namna ambayo atawasumisha madai aua malalamiko yake kuhusu swala Zima la Maadili.