Home LOCAL TMDA YATOA ELIMU KWA WANANCHI MATUMIZI YA DAWA BANDIA SABASABA

TMDA YATOA ELIMU KWA WANANCHI MATUMIZI YA DAWA BANDIA SABASABA

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa elimu kwa Wananchi kuhusu matumizi ya Dawa bandia kwa lengo la kuwajengea uelewa juu ya madhara yanayotokana na Dawa hizo.

Akizungumza kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu JuliausĀ  Nyerere Jijini dar es Salaam, Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma TMDA Gaudencia Simwanza amesema Dawa bandia ni hatari kwa afya ya binadamu, na kuwasihi watanzania kujihepusha na matumizi ya Dawa hizo.

“Dawa bandia zinaweza kusababisha madhara kwa watumiaji kwani inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtumiaji badala ya kumtibu na maisha yake yakawa hatarini, siku zote tunasema ni hatari kwa maisha ya binadamu, madhara ni mengi sana, unaweza kupata ulemavu, au usipone kabisa hilo tatizo na kusababisha ugonjwa mwingine.

“Hivyo basi unatakiwa kwenda kununua Dawa ambazo umeandikiwa na Daktari katika maduka yanayotambulika nakusajiliwa na mamlaka husika” amesema Simwanza.

Ametoa wito kwa wananchi kuwafichua watu wote wasio waaminifu wanaokiuka taratibu kutoa taarifa kwenye Mamlaka hiyo, na kwamba TMD wana utaratibu wa kumlinda mtu anayetoa taarifa za kiuharifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here